Uganda's Daily Monitor raided over Museveni 'plot'

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Polisi nchini Ugandan wamevamia ofisi za magazeti kufuatia taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais.

Vituo viwili vya Redio pia vamiwa na kuzimwa , hii ni kwa muujibu wa gazeti la serikali la New Vision.

Wiki iliyopita magazeti ya Uganda yalidai kuwa kuna njama za kuwauawale watakao pinga mpango wa Rais Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda.

Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji yalitolewa na Mkuu fulani wa jeshi la Uganda.

Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung'atuka uongozini mwaka 2016.

Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni anamuandaa mwanawe Muhoozi Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini kushikilia uongozi wa Uganda.

Lakini serikali ya Museveni imekanusha kwamba kuna mipango kama hiyo.

Mwanawe Museveni Brig. Kainerugaba.

Wiki iliyopita gazeti la, the Daily Monitor,na jengine la , Red Pepper, lilichapisha barua ya siri ikidai ilikuwa imeandikwa na Jeneral David Sejusa, ikitaka uchunguzi ufanywe kuthibitisha madai kwamba kuna mipango ya kuwauwa wote watakaopinga mipango ya Rais Museveni kumpachika mwanawe uongozini.

Uvamizi huo wa polisi umeidhinishwa na mahakama ya Uganda na ulikuwa unalengo la kutafuta barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na mkuu huyo wa Jeshi akifichua njama za mauaji.

Vituo viwili vya Redio vinavyohusiana na Daily Monitor, Dembe FM na KFM, pia vilivamiwa na kuzimwa.

Rais Yoweri Museveni

Mkurugenzi Mkuu wa Daily Monitor Bwana Alex Assimwe aliambia BBC kwamba Chumba chao cha Habari kilivamiwa na polisi wapatao 50 waliojihami kwa silaha.

Lakini wachanganuzi wa maswala ya kisiasa wanadai kuwa ikiwa barua ya Jenerali Sejusa ni ya kweli basi ni dalili kuwa kuna hali mvutano ndani ya jeshi huku ikidhaniwa kuwa wanajeshi wakongwe huenda wanapoteza uwezo kwa wanajeshi chipukizi wanaoongozwa na mwanawe Museveni Brigadia Kainerugaba.

Jenerali Sejusa ni mwanajeshi mkongwe aliyekuwa katika vita vya ukombozi uliyomuweka Rais Museveni madarakani mwaka1986.
Kwa muujibu wa taarifa za AP kamanda mmoja wa jeshi Jenerali Aronda Nyakairima amenukiliwa akisema kuwa Jenerali Sejusa kwa wakati huu anachunguzwa kutokana na barua anayodaiwa kuiandika.

===

English users:

Ugandan police have raided the offices of at least two newspapers following reports that President Yoweri Museveni is grooming his son to succeed him.

Two radio stations have also been taken off air, the state-owned New Vision newspaper reports.

Last week, newspapers reported claims allegedly made by an army general that those opposed to Mr Museveni's son succeeding him risk being killed.

Mr Museveni, in power since 1986, is due to step down in 2016.

There has been long-standing speculation that his son Muhoozi Kainerugaba, a brigadier in the army, is being groomed to succeed him.

The government has denied having any such plans.

'Anarchic'
Uganda's leading private newspaper, the Daily Monitor, and another newspaper, Red Pepper, last week published a confidential letter, purportedly written by army General David Sejusa, calling for an investigation into allegations of a plot "to assassinate people who disagree with this so-called family project of holding onto power in perpetuity".

The police raid was authorised by a court and was aimed at retrieving the alleged letter from the offices of the two newspapers, New Vision reports.

Two radio stations linked to Daily Monitor, Dembe FM and KFM, had also been "switched off", it reports.

Daily Monitor Managing Director Alex Assimwe told BBC Focus on Africa that about 50 armed policemen had raided its newsroom.

"They must be under instructions. It is horrifying that in this day and age you should employ all these methods - shut down a media house to get to a document," he said.

He added that the newspaper did not have the document, and was not compelled to divulge its sources to the police.

"The law protects us," he said.

Analysts say Gen Sejusa's letter suggests a power struggle within the military top brass, as the older generation of army officers gradually loses power to the new guard, of which Brig Kainerugaba is a prominent member, AP news agency reports.

Gen Sejusa fought alongside Mr Museveni when his rebel movement seized power in Uganda in 1986.

Top army commander Gen Aronda Nyakairima said Gen Sejusa was being investigated, AP reports.

His letter "champions the agenda of the radical and anarchic political opposition, hence rendering him partisan", Gen Nyakairima said, it adds.

Gen Sejusa's lawyer Joseph Luzige said his client was out of the country, and would not return at the moment as he risked being arrested, AP reports.

He would stay out of Uganda until his legal team prepares for any potential cases against him, Mr Luzige added, it reports.


===

CHANZO: BBC
 
Taarifa zinazohusiana
Afrika , Uganda , Yoweri Museveni:

Museveni aonya mataifa ya Magharibi
Rais Museveni wa Uganda amelaani hatua ya nchi za magharibi kuingilia kati masuala ya Afrika na kuonya kuwa jambo hilo watalivalia njuga.
Rais Yoweri Museveni
Bw Museveni pia amekanusha madaikuwa Muungano wa Afrika umeshindwa kushughulikia migogoro ya Afrika hususan suala la Libya.
Bw Museveni ameyasema hayo mwishoni mwa juma alipokutana na waandishi habari nyumbani kwake Rwakitura, magharibi mwa Uganda, ambapo amezungumzia masuala mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Mashambulizi
Hii ni mara ya kwanza kwa rais Museveni kukutana na waandishi wa habari wa Uganda na wa kimataifa, tangu achaguliwe tena kuliongoza. Amezungumzia masualambalimbali.
Alizungumzia suala la Libya - ambapo yeye ni rafiki wa Kanali Muammar Gaddafi - inayokabiliwa na upuinzani sio tu kutoka kwa raia wa mashariki mwa nchi lakini pia na mashambulizi ya anga ya Nato.
Bw Myuseveni alisema mashambulizi hayo ni hatua ya mataifa ya Ulaya kujiingiza katika masuala ya Afrika.
Ukoloni mamboleo
Alisema kuwa hii ni hatua mpya wakati huu japo walikuwa wanafanya hivyo wakati wa nyuma.
Ameongeza kuwa Afrika itaweza kushinda watu wanaotaka kuleta alichosema "ukoloni mamboleo kama ilivyofanya kupambana na ukoloni siku za nyuma".
Bw Museveni amesema mataifa ya magharibi yalifanya vibaya kutohusisha Muungano wa Afrika.
Ameonya
Mwandishi mmoja alipendekeza kuwa huenda uingiliaji huo wa mataifa ya magharibi ulichochewa na kujivuta kwa muungano wa Afrika.
Museveni alipinga hoja hiyo, akisema muungano wa Afrika umefanya mengi, kama vile kuipatia uhuru Afrika kusini, kumfukuza Idi Amin kutoka Uganda na pia suala la Libya na Ivory Coast.
Alisema muungano huo ungeweza kutatua suala la Libya.
Aidha ameonya kuwa ikiwa nchi za Ulaya hazitakoma kuingilia kati masula ya Afrika wajitayarishe kwa kile alichoita "Vietnam nyingine".

BY: BBC SWAHILI
 
Taarifa zinazohusiana
Afrika , Uganda , Yoweri Museveni:

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameituhumu mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kile alichotaja kutumia vitisho kama njia ya kuingilia uchaguzi wa Kenya.
Museveni aliyasema hayo wakati akiwahutubia wakenya na wageni waalikwa katika sherehe ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta mjini Nairobi. Miongoni mwa wageniwaalikwa walikuwa marais kadhaa wa Afrika na wanadiplomasia.
Uchaguzi huo ulifanyika mwezi Machi ambapo rais Kenyatta aliwezakumshinda mpinzani wake mkuu Raila Odinga.
Kenyatta na naibu wake Willima Ruto wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya ICC kufuatia ghasia zabaada ya uchaguzi mkuu uliofanyikamiaka mitano iliyopita.
Kenyatta na Ruto wanatakiwa na mahakama hiyo kwani wamesmekana kuwa washukiwa wakuu wa ghasia hizo.
''Nataka kuwapongeza wapiga kura wa Kenya kwa swala lengine moja . Hatua ya kukataa vitisho vya mahakama ya ICC,'' alisema Museveni.

BY: BBC
 
du hizi plitiksi za kiafrika shida tupu....sasa hiyo ni demokrasia au ndo utawala wa kifalme wa kurithishana madaraka??
 
Kuna habari kuwa Rais Museveni wa Uganda amekifungia kituo cha redio cha KFM kwa kuandika habari zinazohusu rais huyo kumwandaa mtoto wake kuwa rais wa nchi pale atakapoondoka madarakani.


Source: The Post Newspapers Zambia - Latest News, Politics, Business, Sports, Photos, Videos » Home News » Museveni closes radio station
 



Uganda Police guard the Monitor Publications Ltd head office in Namuwongo, Kampala on May 20, 2013. Photo/MONITOR









Some of the Monitor Publications Ltd employees who we denied access to their offices on May 20, 2013. Photo/MONITOR








 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…