Uganga wa kienyeji hurithishwaje?

Uganga wa kienyeji hurithishwaje?

Ninja 1

Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
30
Reaction score
12
Habari wana jamvi,

Kama kichwa kinavyosema hapo juu. Je, hurithishwa kutoka kwa babu/bibi kwenda kwa mjukuu au baba/mama kwenda kwa mtoto?

Je, mganga wa kike anaweza kumrithisha wa kiume au vice versa?

Mwenye uelewa wowote tufahamishane.
 
Mshana Jr will advise after Sunday service
Nisamehe Ninja 1 mizimu isije ikaanza kujihami baada ya sentensi ya Kingereza, ikawakumbuka Wajerumani na bunduki zao zilizowafanya leo wawe mizimu pamoja na Kinjekitile wait na dawa yao ya maji
 
Na mimi nitanufaika na hili somo, tuwasubiri wataalamu
 
Kumbe hii nayo huwa ni katika urisi "urithi" ?

Dunia ina mengi.
 
Mambo ya uganga na uchawi yamebadilika sana siku hizi kwani hata ulimwengu wa roho hufuata hali na mwenendo wa binadamu kama vile technolojia, utamaduni n.k.

Siku hizi wapo wengi sana wanakuwa wachawi na waganga wa jadi bila hata kurithishwa na mtu.

Shetani na mapepo yake huwafundisha watu uchawi na uganga moja kwa moja siku hizi.

Ajabu hata watoto wadogo wameingizwa katika uchawi ilhali wazazi wao hawana habari.

Ukitaka kuwa mchawi au mganga ni dakika tu siku hizi. Ila tafadhali mtu asijaribu kwani hakuna utumwa kama huo duniani.
 
Enzi hizo mimi ndio nilikua next in line ya kurithi mikoba ya babu😂😂 sijui ilikuaje lakini mpaka sasa sioni hiyo mikoba.
 
Mambo ya uganga na uchawi yamebadilika sana siku hizi kwani hata ulimwengu wa roho hufuata hali na mwenendo wa binadamu kama vile technolojia, utamaduni n.k.

Siku hizi wapo wengi sana wanakuwa wachawi na waganga wa jadi bila hata kurithishwa na mtu...
Asante mkuu! .. na je kwa wale wanao rithishana, utaratibu ni upi je mganga wa kike anaweza kumrithisa wa kiume? .. nifafanulie kama kuna lolote unalolijua kuhusu hili mkuu!
 
asante mkuu! .. na je kwa wale wanao rithishana, utaratibu ni upi je mganga wa kike anaweza kumrithisa wa kiume ? .. nifafanulie kama kuna lolote unalolijua kuhusu hili mkuu!
Inawezekana kabisa siku hizi bibi akamrithisha uchawi mjuu wake wa kiume, nimeona visa kadhaa mambo yamebadilika na ujanja wa kuzimu umebadilika pia. Tuwe makini.
 
Mkuu ukirithi usimsau mtoto wako mwelevu kumuachia mikoba
 
Back
Top Bottom