Ugatuzi umepunguza idadi ya Wakenya maskini hadi 36%


Mfumo wenu wa sasa ndivyo wa kwetu ulikua miaka ileeee, yaani Tanzania hunikumbusha historia ya Kenya maana kuna kipindi tulikua na

Mkuu wa mkoa
Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa tarafa
Meya
Mbunge wa jimbo
Diwani
Chifu
Mzee wa mtaa
Na wengineo ambao hata siwakumbuki maana tulikua tunafundishwa kwenye somo la uraia (civic education) miaka ile nikiwa shule ya msingi.

Leo hii mfumo umeboreshwa, wataalam waliukalia chini na kuandika katiba mpya, tumeona mafao mengi, tumeona nchi ikibadilika na kuwa ya uchumi wa kati, tumeona hatua zinapigwa kwa mwendo kasi, maendeleo yanamkuta Mkenya wa ngazi ya chini kule mashinani, ni dhahiri hatuna cha kujutia.
Japo pia ni wazi kwamba kuna changamoto si haba, lakini pia wengi tulizitegemea maana kabal ya katiba mpya tulikua tunaishi kwa mazoea.
 
Asili ya muafrica ni uvivu na kualalamika ,ukiona wewe ni mchapakazi na walau unamaendeleo basi ujue ya kwamba mazingira yamekusaidia sana kujiongeza pamoja na elimu ya mkoloni...
Ubinafsi karoho kauchoyo na vijitabia vya hovyo ndio maana hawa watu wa rangi nyeupe wanatucontrol...
Mkute muafrica mchapakazi,aliesoma asie mbinafsi na mpenda maendeleo ya kweli wengi wa Hawa watu wanaroho ya kizungu ...
 

Hapa umechangia kiushabiki bila kufuatilia inavyokua, cha msingi ni kwamba gatuzi zisizokua na chochote zinabebwa na serikali kuu, lakini hilo la kuwapa asilimia ya mapato yao inahamasisha watendaji kwenye kila gatuzi kujituma balaa. Maana kila gavana ameruhusiwa kubuni mikakati endelevu ya kumuwezesha kuongeza mapato, wengi tumeona wakijipeleka Uarabuni na Uchina kuwavutia wawekezaji kwenye gatuzi zao.
 

1. Hapo awali pia sisi tulikua na mfumo kama huwo amabo tulirithi kutoka uingereza. Madiwani, yaani councillors walichagua meya. Tofauti ni kuwa hapo awali, Waziri anayeshughulikia serikali za local government alikuwa ndiye anateua Town Clerk ambaye ndiye alikuwa accounting officer. Tena, Waziri angeweza kudissolve serikali za local government wakati wowote.

La maana kabisa ni kuwa hospitali ziko chini ya serikali za kaunti. Hosipitali mbili tu - Kenyatta na Moi Teaching ndizo ziko chini ya serikali kuu.

Haya ndiyo majukumu ya serikali za Kaunti/gatuzi. Nime copy-paste kutoka kwenye katiba ya kenya.



Sehemu ya 2—Serikali za Kaunti
Mamlaka na kazi za kaunti ni—
1. Kilimo, pamoja na-
(a) Kilimo cha mimea na wanyama;
(b) Viwanja vya kuuzia wanyama;
(c) Vichinjio vya kauni;
(d) Udhibiti wa magonjwa ya mimea na wanyama; na
(e) Uvuvi.
2. Huduma za afya za kaunti pamoja na, hasa—
(a) Vituo vya afya vya kaunti na maduka ya dawa;
(b) huduma za magari ya wagonjwa;
(c) Kuimarisha afya ya kimsingi;
(d) Kutoa leseni na kusimamia shughulia za kuuza vyakula kwa umma;
(e) Huduma za utabibu wa wanyama (isipokuwa usimamizi wa taaluma hii);
(f) Makaburi, kumbi za matanga na tanuu za kuchomea maiti; na
(g) Uondoaji taka, maeneo ya kutupa taka na utupaji taka.
3. Kudhibiti uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa mazingira kupitia kelele, na usumbufu
mwingine kwa umma na utangazaji nje ya makazi.
4. Shughuli za kitamaduni, burudani za umma na huduma za kufurahisha umma pamoja
na—
(a) Kucheza dau, kasino na njia nyingine za kamari;
(b) mashindano ya mbio;
(c) Utaoji leseni kwa pombe;
(d) majumba ya Sinema;
Katiba Inayopendekezwa Ya Kenya • 173
Draft for approval
(e) maonyesho ya video na kukodisha;
(f) maktaba;
(g) makavazi;
(h) michezo na shughuli za kitamaduni na vifaa; na
(i) bustani za kaunti, fuo na nyenzo za burudani.
5. uchukuzi katika kaunti, pamoja na —
(a) barabara za kaunti;
(b) taa za barabarani;
(c) magari na uegeshaji;
(d) usafiri wa barabarani kwa umma ; na
(e) vivuko na bandari, isipokuwa usimamizi wa usafiri majini wa kitaifa na kimataifa
na shughuli zinazohusiana na hizo.
6. Udhibiti na hali ya wanyama, pamoja na-
(a) kutoa leseni kwa mbwa; na
(b) Nyenzo za kuhifadhi, kutunza na kuzika wanyama.
7. Ustawishaji wa biashara na usimamizi, pamoja na—
(a) masoko;
(b) leseni za biashara (isipokuwa udhibiti wa taaluma hizo);
(c) usawa katika shughuli za kibiashara;
(d) utalii wa humu nchini; na
(e) vyama vya ushirika.
8. Mipango na maendeleo ya kaunti, pamoja na—
(a) takwimu;
(b) usoroveya na uchoraji ramani;
(c) mipaka na ujenzi wa nyua;
(d) makazi; na
(e) Uunganishaji na udhibiti wa nguvu za umeme na gesi.
9. Elimu ya chekechea (Wabongo mnasema shule za awali), elimu, vyuo vya ufundi anuwai, vituo vya utengenezaji wa
vyombo vya kinyumbani na nyenzo za utunzaji wa watoto.
174 • Katiba Inayopendekezwa Ya Kenya
Draft for approval
10. Utekelezwaji wa sera maalum za serikali ya kitaifa kuhusu maliasili na uhifadhi wa
mazingira, pamoja na—
(a) uhifadhi wa udongo na maji; na
(b) misitu.
11. Huduma za kazi kwa umma katika kaunti pamoja na —
(a) mfumo wa usimamizi wa maji ya tufani katika sehemu za majengo; na
(b) huduma za maji na usafi.
12. huduma za kuzima moto, na usimamizi wa majanga
13. udhibiti wa dawa na ponografia.
14. kuhakikisha na kusimamia ushiriki wa jamii na sehemu za mashambani katika
utawala wa viwango hivyo vya mashinani na kuzisaidia jamii pamoja na maeneo
hayo kujenga uwezo wa kiusimamizi ili kuwezesha matumizi ya mamlaka na
majukumu na kushiriki katika utawala wa mashinani.
 

Haha..umenikumbusha tarafa. Hili jina nimelitafuta sana. Halafu umewacha wapi Kata na Kata ndogo. Nakumbuka somo la Geography History and Civics;

Darasa la kwanza - Our School
Darasa la Pili - Sikumbuki
Darasa la tatu - Our District - Kakamega
Darasa la nne - Our Province Western
Darasa la tano - Our Nation - Kenya
Darasa la Sita - Kenya and the rest of Eastern Africa (Kenya, Uganda, Tanzania, Ethiopia, Sudan na Somalia)
Darasa la Saba - Kenya and the rest of Africa
Darasa la Nane Kenya and the Rest of the world

Wiki chache zilizopita nimetoka shule fulani hapa nikapata maswali haya kwenye ubao

1. Who was the first vice president of Tanzania
2. When did Tanganyika unite with Zanzibar?
3. Name three national philosophies
 
Hakuna kitu hapo rafiki. Hakuna ubora wowote hapo Labda ungeeleza tofauti ya sisi tulivyo sana na mnavyojidai umeboreshwa
 
Naona unaongea mbwembwe tu rafiki. Hakuna hata cha maana chochote.
Wewe nimekuambia unipatie tofauti ya mfumo wenu "Mnaousema wa kisasa" Na huu mfumo wetu.
Hapa siongelei majina bali naongelea utendajikazi.
 

Dah! Halafu nilikua nachora mkoa wangu wa Bonde la ufa hadi raha, nakumbuka mwalimu wangu wa GHC Mr. Ingwero alihakikisha kila mmoja wetu anachora ramani ya Kenya na mikoa yote nane, kiboko kilikua kinatembea mpaka ramani inajichora yenyewe.....yaani darasa lote tunataharuki, hakuna aliyekua anadiriki kutabasamu.
Hatukua tunatoka nje kwenye vipindi vya mapumziko, unakuta kila mtu anachora na kuchana karatasi kila akikosea, mwalimu hayupo ametuaga hadi kesho lakini wenyewe inabidi tujitume balaa, maana hiyo kesho ikifika jamaa ataingia darasani amenuna na kulianzisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…