Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Zoezi la ugawaji wa vizimba kwa wafanyabiashara wa soko la Mbuyuni umezua sintofahamu baada ya baadhi ya wafanyabiashara kudai kutoorodheshwa kwenye majina ya wanaostahili kupewa vizimba .
Soko hilo ambalo ni moja ya soko makubwa ndani ya manispaa ya Moshi ,liliungua mwaka Jana na kuleta hasara kubwa ya mali za wafanyabiashara kabla ya serikali kulijenga upya.
Sasa baada ya manispaa ya Moshi kutuma wataalamu na kufanya vipimo baadhi yao wanadia ni vidogo huku baadhi wakidai majina yao hayaonekani.
Ilibidi Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe kuingilia kati na kuweka mambo Sawa ikiwamo kuingiza baadhi ya wafanyabiashara ambao majina yao hayakuwa yameingizwa kwenye orodha ya awali.
Baada ya majadiliano ikaamuliwa meza zitakazojengwa ni zenye ukubwa wa 120×80 kutoka ukubwa wa 120×90.
Akijibu malalamiko ya ufinyu wa Eneo,Nasombe amewataka wale wenye uhitaji wa Eneo kubwa waende kwenye masoko ya Bomambuzi,soko la Kati,STENDI kuu ya mabasi na maeneo mengine.
Soko la Mbuyuni linajumuisha wafanyabiashara wa nyanya,mama Lishe,vitunguu,vazi.samaki,Nyama,matunda na bidhaa mchanganyiko.
Mpaka sasa vizimba 756 vimepimwa wakati idadi ya wafanyabiashara ikikadiliwa kuwa 920.
Mengine ni hapo baadae