Wewe ulidanganywa, na ni afadhali umesema kuwa ulikuwa hujazaliwa kwa vile unamfahamu Maelecela leo kwa sababu ya Nyerere; wangekuwa na ugomvi basi hata jina la Malecela ungekuwa hulijui kabisa katika siasa za leo kwa kuwa Nyerere alikuwa na uwezo wa kufuta wanasiasa kabisa, wapo wengi sana waliofutwa na Nyerere. Malecela aliendela kutumika kwenye serikali ya Nyerere kwenye ngazi za juu sana serikalini mapungufu yake kwa muda mrefu sana hadi Nyerere alipostaafu. Hata hivyo Nyerere alikuwa anajua mapungufu yake ndiyo maana akasema kuwa mtu huyu hana uwezo wa kuwa rais. Kusema kuwa hana uwezo wa kuwa rais siyo kuwa walikuwa na ugonvi, ingawa Malecela na wafuasi wake walilichukulia hilo kama ugomvi, na inawezekana ndio wanaokupa taarifa hizo kuwa Nyerere alikuwa na ugomvi na \Malecela.