kweli kaka ila tatizo ni pale kaugomvi kadogo tu kanapotokea basi kwangu ni kitu kingine kabisa,labda kuna tofauti ya ugomvi kutoka nyumba moja hadi nyingine,kwetu ilikuwa tofauti kidogo unaposhuhudia mtu anapigwa kipigo cha paka mwizi kisa amezima taa kabla mume hajarudi,au amezidisha kunywa vidonge toauti na maagizo ya dr naomba unielewe kidogo hapo
unamaanisha nini unapo sema mbela yako, wakiwa chumbani utaacha waumizane wakati unasikia wanagombana ???
sidhani maana huwa kuna hali fulani inanipata,mpaka nikija shtuka nishampeteza mtu muhimu sana,mimi mwenyewe ndio huwa najiona kuwa hawastahili kuwa nami maana nitawatoa kwenye mstari,ila ni tatizo nadhani wazazi wangejua wanatengeneza bomu gani kwa watoto zao wangefanya kila namna kuacha ugomvi wa kiloa siku,ndio yashamwagika kaka hayazoleki
HABARI WAKUBWA ZANGU. NIMEKUJA HAPA MNISAIDIE INAPOTOKEA BABA NA MAMA WANAGOMBANA, MIMI KAMA MTOTO NARUHUSIWA KUWA REFA??.
1. JE NI HAKI NIKAINGILIA UGOMVI KATI YA MAMA NA BABA??
2. SOME TIMES NAJUA KUWA MAMA NDO AMEKOSEA LAKINI SIWEZI MWACHA MZEE AENDELEE KUMWANDAMA MOTHER. NIFANYAJE HAPA NAPO
3. JE HATA KAMA NIKIINGILIA, NIFANYAJE ILI NISIPENDELEE UPANDE MMOJA UKIZINGATIA KUWA NAMPENDA MAMA KULIKO BABA NA HII IMETOKEA HATA SIJUI KWA NINI.
NAOMBA MASAADA WENU.
Inategemea ni ugomvi gani na umetokea wapi, lakini kwa kifupi kuna ugomvi wa kutofautiana kwa kauli tu yani kuzozana, kitu ambacho watoto hawarusiwi kuingilia, na kuna ugomvi wa ngumi, ambao pia labda wapigane mbele yako ndo waweza ingilia na kuamua. Nachosema hapa inategemea inatokea wapi na wakati gani, kuamua unaweza ila si kuingilia, sometimes wazazi wetu wanahitaji ushauri wetu.
infact mkiwa kama wazazi(watu mliokwisha kuwa na familly) haipendezi kugombana mbele ya watoto wenu,,,,na tabia hii hujengwa tangu siku ile mnaoana kuwa kama mke na mume,,,ukizingatia hakuna wasio gombana katika ulimwengu huu,,,sasa basi kiachotokea na kuzingatiwa ni pindi mmoja wenu tuu anapokosea maybe kimfano tuu,,,,,
mmekaa kimazungumzo pengine wewe ni wakiume na kuna nduguzako mama ako hata wageni tofauti na hao akatokea mkeo kusema neno halikukufurahisha bali ni kukughadhibisha unachotakiwa kufanya nikuondoka na kumuita yeye chumbani huko ndio mtamalizia mambo yenu,,,na mkijijenga kihivyo basi wallah hakuna ugomvi utakaotokea mbele ya watoto wenu na kuzitesa nafsi zao,,,,
na kiupande wa mada ni kuwa mtoto haruhusiwi kuingiza neno lake pindi wazazi wake wanapogombana ispokuwa tuu kwa sababu muhimu,,,ikiwa yeye ndio aliekuwa chanzo cha ugomvi wao,,,kutetea na kusema hata uongo ilimradi kuwapatanisha,,,kwani uongo wa kupatanisha watu wawili waliokuwa wameghadhibiana nafsi zao huo umeruhusiwa kwa dini ya kiislam... shukran .....
hapa sijakuelewa unamaanisha nini dada NR,na kiupande wa mada ni kuwa mtoto haruhusiwi kuingiza neno lake pindi wazazi wake wanapogombana ispokuwa tuu kwa sababu muhimu,,,ikiwa yeye ndio aliekuwa chanzo cha ugomvi wao....
Mtoto kacheze zako huko, mtoto wangu simruhusu aingilie kama ambavyo sintaruhusu afahamu tuna ugomvi na mamake.
hapo kulikuwa hakuna mapenzi ya kweli, na pia may be ni yale ya kizamani ya kuchaguliwa mke au mume na wazazi. Unayempenda kwa dhati ya moyo wako huwezi kumpa kichapo cha paka mwizi hata awe amekuudhi kiasi gani. Na pia tabia hiyo ipo kule kanda ya ziwa wanakotokea maafande wengi, tafadhali sijataja jina wala kabila.kweli kaka ila tatizo ni pale kaugomvi kadogo tu kanapotokea basi kwangu ni kitu kingine kabisa,labda kuna tofauti ya ugomvi kutoka nyumba moja hadi nyingine,kwetu ilikuwa tofauti kidogo unaposhuhudia mtu anapigwa kipigo cha paka mwizi kisa amezima taa kabla mume hajarudi,au amezidisha kunywa vidonge toauti na maagizo ya dr naomba unielewe kidogo hapo
Binafsi sidhanini kitu chema kuingilia ugomvi wa wazazi. Labda kama mtoto mwenyewe unayetaka kuingilia ni mtu mzima mwenye uelewa wa mambo ya mahusiano. Wazazi wote ni wako na una uchungu nao wote utaingilia vipi? Kama ni mtoto wa umri mdogo basi tafuta msaada wa watu wazima lakini wewe jiepusha kabisa.
Hapana simaanishi kuingilia kumchangia mmoja, huezi ona mzee anampiga mama mpanga anamvulisha nguo usiamue au kuwagombeza ikibidi, japo ni wazazi kwenye haki inabidi uisimamie haki, kama wanafanya upuuzi una wambia tu.
Je hii ni ipo kwenye haki za watoto???