Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Ila Mbowe amepitia mengi sana!
Jioni moja pale Bungeni kwenye Ukumbi almaarufu sasa wa Msekwa uliibuka ugomvi wa maneno ya kejeli baina ya Waziri wa Elimu na Utamaduni kipindi hicho bwana Kapuya na bwana Mbowe uliopelekea wakubwa wale nusra wazichape.
Kisanga kilianza pale Mbowe mchango wake ulipojikita kutetea mila na desturi zetu za Kiafrika huku akiituhumu Wizara ya Elimu na Utamaduni chini ya Kapuya kutokushtushwa na kumomonyoka kwa maadili ya vijana wetu kutokana na utandawazi.
Naye Waziri Kapuya akijibu shutuma zile alimkejeli Mbowe kwa kuharibu mila na desturi za vijana wengi wa Kitanzania kwa kuwafungia ndani ya ukumbi wake wakati huo uliofahamika kwa jina la Billicanna na kuwafundisha usasa na kwalo hakuwa na haki ya kuituhumu W ELNU. Vilevile Waziri Kapuya alimtuhumu Mbunge Mbowe kwa uzinzi na uasherati na mabinti wadogo waliokuwa wakienda ukumbini pale.
Baada ya majibu ya Kapuya nakumbuka Mbowe alifula kama mbogo hali iliyopelekea utulivu Bungeni kupotea.
Wangapi tunakumbuka kisa hicho?
Paskali naamini unakumbuka!