Ugonjwa gani huu nisaidieni wanaJf

Nic1987

Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
19
Reaction score
2
Vipele vigumu kwenye uume vimenitokea havitoi maji wala vitu vyeupe alafu nivigu vinakwaruza nimeenda kupima. Nikapimwa vipimo vya RPR majibu nikapewa NON REACTIVE nikapima na PITC majibu yakaja SN sana na doctor akaniambia hakuna tatizo nisaidie wapenda hata mapenzi naona aibu kufanya kwa sababu ya vile vimenianza tang mwaka jana mwezi wa 7 nitashukuru kwa ushaur wenu au nitumie dawa gani?
 

weka picha kwanza halafu tuone ukubwa wa tatizo ndio tunakuambia dawa
 
Nieleweshe ndugu yangu dah!naogopa hata kuchukua demu
 

Nadhan ndo umetahiriwa hivi karibun, hivyo ni kawaida kutokea ukitahiriwa...ni design km chunusi hivi vyeupe ila havitumbuki.
 
viko sehem gan ya uume mkuu!? kwenye shina, ring au kichwa? maana pale kwenye ringi vpo vidogo vidogo vgumu vya kawaida tu!
 
Mimi nimetahiri tangu nikiwa na miaka 3 na sasa 27
 
Vipo kwenye shina na karibu na ring mkuu havitoi chochote vigumuu nikiviminya sana vinatoa damu
 
Kwa maelezo yako vinaweza kuwa ni GENITAL WARTS. Hii genital warts ni upele unaota lkn sio upele kamili ni km uvimbe unaota km ua hivi then unasambaa sehemu za haja kubwa. Ni ugonjwa wa zinaa ambao hutokana na mtu kuwa na multiple partiners. Na ugonjwa huu husababishwa na virus vinavyoitwa HUMAN PAPILOMA VIRUS TYPE 6, au 16, 32 na pia zipo virus type nyingine. Kwa kawaida mwanamke anaweza kupata hivi virus na akawa anavisambaza pale anapokuwa na mahusiano na wanaume tofauti. Hivyo kuueneza ugonjwa, na mara nyingi wanawake hupata cervical cancer au genital warts ambayo husababishwa na hivi virus na mwanaume hupata pia na pia huweza kusambaa hadi kwenye puru na kusababisha cancer ktk njia ya haja kubwa.
Matibabu ni kuvikata hivi vipele na kupaka cream au poweder iitwayo podophyllin.
Pia epuka wapenzi wengi kuepusha maambukizi mapya ama kuwaambukiza ambao hawana.
Huo ndio mchango wangu.
 
53930dah!nashukuru sana sana nilikuwa sijui ndugu yangu ila kwenye ------ au puru hakuna viko kwenye uume tu
 
Ndio future ebu waeleze kabisa mi sina raha kabisa nimekuwa muoga
 
53930*** cream aina gani na inapatikana maduka ya dawa au!
 

Dokta kakwambia hamna tatizo unataka nini zaidi?
 
Pole bhana ila jitahidi kufanya ngono salama!
maana inaonekana ww ni mtu wa sketi kiasi flan...!
samahan lkn
 

Pole sana kwa hayo yaliyo kukuta na mimi nina changia kama walivyochangia Wenzangu

jambo la kwanza ningelikushauri uende Hospitali ya Muhimbili kupima tena mkojo na Damu yako ndipo

itajulikana unamwa ugonjwa gani? Kisha uje hapa utupe maelezo unaumwa kitu gani? Mimi

ninahisi una umwa moja kati ya haya maradhi mawili.


Herpes



Huu husababishwa na aina fulani ya kirusi, kama kile kinachosababisha mafua na vidonda vya mdomoni. Mbali na kusambazwa kupitia ngono pia husambazwa kupitia kufanya mapenzi ya
kunyonyana sehemu za siri.

Dalili: Ni Kupata vidonda ukeni au uumeni mfano wa vile vinavyotokea mdomoni wakati wa homa kali ya mafua.

Matibabu: Sasa kuna dawa na krimu za kupambana na virusi hivi. Lakini kumbuka hata unapotibiwa virusi vya herpes bado hubaki mwilini mwako na vinaweza kuzusha tena vindonda.

Pia kama umja mzito unaweza kumwambukiza mtoto wako, hivyo basi kama una vijidonda ni vyema kumjulisha mkunga wako ama daktari ili upate matibabu yafaayo.




Kaswende (Syphilis)





Ugonjwa huu nao husababishwa na bacteria Treponema Pallidum
Dalili zake hazionekani kwa urahisi. Huenda ukaanza kwa kijidonda au kipele kwenye uke au

uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa. Kidonda hiki kinapopona usidhani ndio mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimya kimya kwa miaka mingi!

Matibabu: Ni bora daktari kufanya uchunguzi wa damu kwani majimaji ya ukeni au uumeni huenda uchunguzi wake usionyeshe viini vya kaswende. Kaswende ni hatari, kama haitibiwi,

inaweza kusababisha utasa au ugumba, na hata kuathiri moyo, mishipa ya damu, ngozi ya mwili, mifupa na hata ubongo na kurukwa na akili.

Hata hivyo matibabu yake ni rahisi – Zipo dawa aina (antibiotics) zinazoweza kutibu kaswende kabisa. Ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo ni vyema mpenzio nae pia atibiwe.

PIA ACHANA NA ZINAA.................
 
Jamani asanteni mimi sio mtu wa kichupi matatizo humtokea mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…