Ugonjwa nisioufahamu

gosikulu

Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
71
Reaction score
51
Ndugu zangu salamu!! Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu ,baba yangu mzazi anaugua ugonjwa ambao umemsumbua kwa takribani miaka miwili sasa,kwanza mguu mmoja unakufa ganzi kuanzia kwenye paja mpaka vidoleni,pia inaambatana na maumivu makali anapokanyaga,alienda hospitali baada ya maelezo wakampa dozi ya mwaka mzima ya ukoma ,akaitumia mpaka akamaliza lakini hali bado ni ileile,ndugu zangu naomba msaada nini nifanye kwa wajuzi wa haya mambo ili niweze kumsaidia mzee wangu,mbarikiwe nyote
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana kwa kuuguliwa. Mlienda hospital gani na mara ngapi? Ameonana na ma-dr bingwa? Nauliza kwa sababu kulingana na maelezo yako inaonekana kama hamjahudhuria hospital mara nyingi. Kuna magonjwa mengine yanajificha na inatakiwa mgojwa afanye vipimo vingi kabla hayajagundulika. Nadhani ushauri ni kumpeleka tena hospital aonane na madaktari na afanye vipimo.
 
Nerves deformities tuu hizi, mpeleke kwa madaktari bingwa atapata tiba sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…