Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Watoto wanne wa familia moja wakazi wa Mtaa wa Sanungu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, wamefariki ghafla kwa ugonjwa usiojulikana hali iliyosababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo na kuiomba Serikali kupitia wataalamu wa afya kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha vifo hivyo.
Gondi Darusi (36) ambaye ndiye baba wa watoto hao anasema; "Alianza kuumwa mwanangu wa kwanza tukaamua kumpeleka kwenye zahanati hiyo ili apatiwe vipimo ambapo ilibainika anaumwa kichocho akapatiwa dawa kisha tukarudi nyumbani na ndipo alipoanza mwingine."
Kwa upande wa mama wa watoto hao, Minza Masuka, amesema baada ya mtoto wao wa kwanza Emmanuel Gondi (13) kurejeshwa nyumbani hakupata nafuu huku wa pili Baraka Gondi (11) alikuwa anadai kuumwa kichwa huku jasho likimtoka.
Mama huyo amesema, waliamua kuwapeleka Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa ajili ya vipimo zaidi lakini hali yao iliendelea kuwa mbaya wakidai kuwa wanaishiwa nguvu.
"Nilipofika nyumbani niliamua kuwachukua mtoto wangu wa tatu na wa nne ambao ni Masuka Gondi(11) na Kiyumbi Gondi (6) kuwapeleka Somanda lakini baada ya kuwafikisha hali zao hazikuwa nzuri hadi kupatwa na umauti.”
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
Credit :itv