Alvin_255
JF-Expert Member
- Oct 26, 2015
- 246
- 503
Ni ugonjwa ambào mtu anakuwa na hisia za Ubinafsi ndani yake, Aina hii ya ugonjwa mtu anakuwa na uhitaji mkubwa wa kusifiwa na kupongezwa katika kile anachokifanya..
Mtu mwenye ugonjwa huu huwa na hisia zilizokithiri za kujiona kuwa yeye ndio wa muhimu hivyo huhitaji kupewa umakini. Watu wenye ugonjwa huu wanaweza kukosa uwezo wa kuelewa na kujali hisia za watu wengine, Ni aina ya watu wanaotamani sifa na uangalizi wa nje.
Aina hii ya watu wenye ugonjwa huu wanaweza kukosa furaha na kukatishwa tamaa ikiwa hawatapokea sifa wanazoamini kuwa wanastahili kuzipata kutoka kwa watu.
Ugonjwa huu unaweza kusababisha matatizo katika maeneo mengi ya maisha ya mtu, ikiwa ni pamoja na: kazini, shuleni, mahusiano ya kijamii, familia nakadhalika.
Kitaalamu Mtu mwenye ugonjwa huu huitwa (Narcissist).
DALILI ZA UGONJWA WA AKILI (NDP).
• Mtu ugonjwa huu huamini kwamba yeye ni wa kipekee hivyo anapaswa kushirikiana na watu wengine wa hadhi kubwa ya kimaisha.
• Huhitaji mara kwa mara umakini, uthibitisho, na sifa kutoka kwa watu wengine.
• Narcissist Huhitaji kutambuliwa kama mtu bora zaidi hata kama hana mafanikio yoyote yale.
• Narcissist Hutumia faida ya watu wengine kupata kile anachokitaka.
• Narcissist Husitiza kuwa ana kila kitu kilicho bora zaidi - kwa mfano, gari, nyumba, au ofisi hata kama hana.
• Narcissist Huwa na papara au hasira wakati ambapo hapewii utambulisho maalumu.
• Narcissist Hujaribu kuwadharau watu wengine ili aonekane kuwa yeye ni bora zaidi.
• Huwa na hali ya kujiona na kutaka kutambulika kwa watu kuwa ana nguvu, akili, uwezo kuliko watu wengine.
• Huwa na Tabia ya kutia chumvi au kusema uongo kuhusu mafanikio, ujuzi au kipaji chake wakati hana lolote au hakuna anachokijua.
• Huwa ni mwenye hisia za kujiona kuwa anastahili zaidi kuliko watu wengine.
• Huwa na hisia za kuwachukia watu wengine Ikiwa hawatamsifia au hawatakisifia kile anachokifanya.
• Hali ya kuhisi kuwa kila mtu anataka kuzingatia matakwa yake, Ikiwa hatafanya Hivyo anamchukia.
• Ukosefu wa huruma au hali ya ubinafsi na kutojali kwa yale ambayo wengine wanapitia au kuyahisi.
SABABU ZA UGONJWA WA AKILI NPD.
Haijulikani ni nini husababisha ugonjwa wa NPD, Lakini Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na mchanganyiko wa mambo ambayo ni pamoja na:
1️⃣ Mazingira — Mahusiano ya malezi ya mzazi na mtoto yenye ukosoaji mwingi kupita kiasi ambao haulingani na uzoefu wa mafanikio halisi ya mtoto, kubembelezwa au kusifiwa kupita kiasi wakati wa malezi, kubaguliwa wakati wa malezi, Kutelekezwa Nakadhalika.
2️⃣ Historia ya familia - Sifa za kurithi, kama vile tabia fulani Kutoka Kizazi hadi kizazi ni miongoni mwa sababu ya ugonjwa huu.
3️⃣ Maumivu ya utotoni (kama vile unyanyasaji wa kimwili, kingono na matusi, ukatili ni miongoni mwa sababu pia).
KATIKA UHUSIANO.
• Kuwa katika uhusiano na mtu ambaye ana tatizo la ugonjwa huu inaweza kuwa changamoto kwako kuishi nae. Narcissist huwa na hitaji la kusifiwa na hisia za juu za kujiweka yeye ndio kipaumbele unayepaswa kumzingatia wakati wote.
Anaweza asionyeshe huruma wala kujali hisia au Maumivu yako tofauti na vile anavyotaka yeye kutoka kwako.
MATIBABU YA UGONJWA WA AKILI NPD
Tiba ya saikolojia/ Ushauri nasihi kutoka kwa mtaalamu wa Matatizo ya Kisaikolojia ina uwezo wa kumsaidia mtu aliye na ugonjwa huu kukuza ujuzi na mikakati ambayo inaweza kumsaidia kubadilisha jinsi anavyohusiana na watu wengine na yeye mwenyewe.
Changamoto ni kwamba watu walio na tatizo hili wengi wao huwa hawatafuti matibabu mara kwa mara mpaka pale ugonjwa huo uanze kuathiri maisha yao.
Watu walio na ugonjwa huu ikiwa hawatashughulikia tatizo lao wana uwezekano mkubwa wa kukuza hali zingine za afya ya akili kama vile: ugonjwa wa wasiwasi, huzuni Pamoja na shida ya matumizi ya pombe au dawa za kulevya.
Ikiwa umetambua dalili na ukaona zinakuhusu, fikiria kuwasiliana na mtoa huduma afya ya akili( Mwanasaikolojia/ mshauri nasihi) ili uweze kupata matibabu sahihi yatakayokuwezesha kuwajibikia tatizo lako ili kuyafanya maisha yako yawe yenye kufurahisha zaidi na yasiywe kikwazo kwa watu wengine.