Kitia umesema"Mpaka sasa familia yangu imeathirika na wazee wawili, na nafahamu familia zingine tatu ambazo wazee wao wamekumbwa na ugonjwa huo."
Kwa hiyo utakuwa una uzoefu mkubwa -unaweza kutusaidia jinsi ulivyowasaidia hao wazee wako na jinsi ulivyousimamisha usiendelee bila dawa kama ulivyosema?Asante.
Kwa bahati mbaya, mzee mmoja alipoanza kuugua, tulijua kuwa amechanganyikiwa kwa ajili ya uzee. Hali iliendelea hivyo hivyo na kwa bahati mbaya akafariki. Kwa sababu hapakuwa na diagnosis ya kutosha, wala autopsy, hatukuweza kujua kwa uhakika kuwa ni kitu gani kilichomuua. Ilikuwa ni rahisi zaidi kuona dalili hizo kwa mzee wetu wa pili. Tulimleta kututembelea huku ughaibuni, ndio tukagundua kuwa tabia yake imebadilika kabisa, anasahau sana, na mara nyingi matamshi yake hayaleti maana. Hapo ndipo tukampeleka hospitali, akafanyiwa medical check up, psychiatric analysis na pia kufanyiwa MRI scan ya ubongo. Vipimo vilionyesha kuwa tayari ameshambuliwa na huo ugonjwa wa alzheimer. Daktari alitueleza hakuna dawa za ku reverse effects za ugonjwa huo, ila kuna dawa amabazo zinaweza kufanya ugonjwa huo usiendelee zaidi. Kwa mfano, hataacha kusahau, lakini rate ya kusahau itabakia palepale, badala ya kuendelea. Mojawapo ya dawa hizo ni Vitamin E (IDO-E9) pamoja na Arisept, au Doneratio, dawa ambazo mpaka sasa anatumia. Hata hivyo, dawa hizo, hasa hizi mbili za mwisho hazipatikani Tanzania, na imebidi tuwe tunatuma kila mara. Hizo anatakiwa kunywa maisha.
Care ya mgonjwa wa alzheimer ni ngumu sana kwa mgonjwa, na wewe unayetoa huduma. Kisaikolojia ita ku affect sana ukiona mzazi wako amebadilika amekuwa na hali hiyo. Mara nyingi atakuudhi kwa maneno yake, na inahitaji uvumilivu na upole katika kutoa huduma. Vilevile kuna haja ya kumpatia mgonjwa mental exercises ili aweza kutumia ubongo. Michezo kama karata, bao nk husaidia. Vile vile inabidi kumpa majukumu ya kufanya kutokana na uwezo wake.
Kutokana na kwamba ugonjwa huu umeanza kuonekana kwetu, kuna haja ya kuelimisha umma kuhusu athari zake. Vilevile kuipa sekta ya afya uwezo wa ku diagnose na kutoa matibabu, ambayo inabidi kupata dawa hizo kwa bei nafuu. Kama nilivyosema awali, kuna haja ya kuangalia jinsi sheria itakavyowalinda watu waliathirika na ugonjwa huu.