Ugonjwa wa fizi kumumunyika na kuacha meno wazi

Ugonjwa wa fizi kumumunyika na kuacha meno wazi, je unaitwajwe na je unatibika?

Msaada wenu wadau.

CC MziziMkavu

Chanzo na Madhara ya Ugonjwa wa Fizi​

Kuna mambo kadhaa yanayochangia kupata ugonjwa wa fizi. Utando wa bakteria ambao kwa kawaida hutokea kwenye meno ndicho chanzo kikuu. Usipotolewa, bakteria husababisha kuvimba kwa fizi. Hatua hiyo inapoendelea, fizi huachana na meno, na hivyo utando huo wa bakteria husambaa na kuingia chini ya fizi. Bakteria zinapofikia hatua hiyo, uvimbe huendelea kuharibu mifupa na fizi. Utando huo, iwe uko juu au chini ya fizi, unaweza kuwa mgumu na kuwa ukoga. Ukoga pia una bakteria, na kwa kuwa ni mgumu na hushikamana na meno, hauwezi kutolewa kwa urahisi kama utando. Hivyo, bakteria huendelea kuharibu fizi.

Kuna mambo mengine pia yanayochangia ugonjwa wa fizi. Yanatia ndani uchafu mdomoni, madawa yanayopunguza kinga mwilini, magonjwa yanayosababishwa na virusi, mkazo, kisukari, kunywa pombe kupita kiasi, kutumia tumbaku, na mabadiliko ya homoni kwa sababu ya mimba.

Ugonjwa wa fizi unaweza kukuathiri kwa njia nyingine pia. Maumivu mdomoni na kung'oka meno kunaweza kupunguza uwezo wako wa kutafuna chakula na kukifurahia. Pia, unaweza kuathiri matamshi na sura yako. Vilevile utafiti umeonyesha kwamba usafi mdomoni unahusiana na afya ya mtu kwa ujumla.

Kutambua na Kutibu Ugonjwa wa Fizi​

Unawezaje kujua kama una ugonjwa wa fizi? Huenda ukaona baadhi ya dalili zilizotajwa kwenye makala hii. Ukiziona ni vizuri kumwona daktari maalumu wa meno ili achunguze fizi zako.

Je, ugonjwa wa fizi unaweza kutibiwa? Inawezekana kuutibu katika hatua za kwanza. Ugonjwa wa fizi unapoenea sana, basi lengo ni kuuthibiti ili usiendelee kuharibu mifupa na fizi zinazotegemeza meno. Madaktari wa meno hutumia vifaa vya pekee vinavyoweza kuondoa utando na ukoga kwenye meno, iwe ni chini au juu ya fizi.

Hata ikiwa si rahisi kwako kupata matibabu ya meno, unaweza kuzuia ugonjwa huo hatari usikupate. Kusafisha mdomo vizuri na kwa ukawaida ndiyo njia bora zaidi ya kuzuia ugonjwa wa fizi.



USAFI WA MDOMONI



Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku. Huenda watu fulani wakahitaji kupiga mswaki mara nyingi zaidi, labda kila baada ya kula, ili kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa fizi

Tumia mswaki ulio laini, na upige mswaki taratibu, na kwa karibu-karibu



Toa uchafu katikati ya meno kila siku ukitumia uzi mwembamba wa pekee, au ikihitajika mswaki maalumu na vijiti vya kutoa uchafu katikati ya meno.Nenda kamuone Daktari. Mkuu@
MIKIDADI KAPAYA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…