Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Ini ni Kiungo Muhimu Sana kwenye mwili wa binadamu ambacho hufanya kazi zaidi ya 500.
Kutokana na sababu mbalimbali Kama matumizi ya dawa yasiyo zingatia ushauri wa wataalam, unywaji mkubwa wa pombe pamoja na maambukizi yanayo sababishwa na virusi, ini hupata shida ya Kuvimba na kutengeneza makovu hivyo kushindwa kufanya kazi vizuri. Hali hii huitwa homa ya Ini au Hepatitis.
Ugonjwa huu huonekana kwa aina tano ambazo ni homa ya Ini aina A, B, C, D na E.
Aina B na C ndiyo hatari zaidi kuliko aina zingine. Mathalani, aina B huwa na uwezo wa kushambulia na kuambukiza mara 50 -100 zaidi kuliko VVU.
Unaweza kupata ugonjwa wa homa ya ini aina B au C kwa kupokea damu na mazao yake kutoka kwa mgonjwa, kushiriki tendo la ndoa, kushirikiana vitu vyenye ncha kali kama sindano pamoja na maambukizi ya mama kwa mtoto wakati wa kujifungua.
Namna pekee ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya ini ni kupitia chanjo. Aidha, ugonjwa huu hutibiwa kwa kutumia dawa mbalimbali za virusi kulingana na aina husika anayokuwa nayo mgonjwa kwa wakati huo.
Kwa mujibu wa ripoti ya July 27, 2022 iliyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Zaidi ya watu milioni 91 wanaishi na aina B au C ya ugonjwa wa homa ya ini barani Afrika huku zaidi ya watu 200,000 wakipoteza maisha kila mwaka.
WHO