Ugonjwa wa Homa ya Manjano walipuka Kenya, watatu wafariki, 15 wagonjwa

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Kenya imetangaza mlipuko wa homa ya manjano baada ya watu watatu kufariki dunia na kubainika wengine 15 wanashukiwa kuambukizwa katika kaunti ya Isiolo, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wizara ya Afya inasema imetuma jopo la wataalamu wa kushughulikia suala hilo kwa haraka. Wizara ilisema pia kuwa itaweka kipaumbele katika utoaji wa chanjo katika kaunti nyingine zipatazo sita, zilizo jirani na Isiolo ambazo pia zinashukiwa kuwa na maambukizi.

Taarifa za vyombo vya habari nchini Kenya zinaeleza kuwa watu wa kwanza wenye maambuki ya homa ya manjano walibainika katikati mwa Januari mwaka huu katika maeneo ya Merti na Garbatullah, hivyo kuzua maswali ni kwa nini hali ya tahadhari imetolewa Jumamosi Machi 5, 2022.

Lakini hayo ni maeneo ambayo ni vigumu kufikika ambako familia ni za wafugaji huku wakihama kutoka eneo moja hadi lingine kutafuta malisho ya mifugo na maji. Vituo vya afya vina wafanyakazi wachache na vitendea kazi vichache pia.

Homa ya manjano ni hatari inayoenezwa na mbu. Dalili zake ni pamoja na homa kali, kichwa kuuma, mdomo kuwa mchungu na wakati mwingine ini kushindwa kufanya kazi.

Pamoja na chanjo ya homa ya manjano kupatikana katika hospitali za serikali, idadi ya watu waliochanjwa ni ndogo, moja ya sababu ni gharama ya chanjo ambayo inafikia dola za Marekani 18 hadi 20, ambazo ni nyingi kwa watu wengi wa Kenya hususan wa vijijini.

Mlipuko wa mwisho wa homa ya manjano nchini Kenya ulitokea 1992/1993


Source: BBC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…