Ugonjwa wa kimeta waua mmoja, 84 hoi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Daniel Mjema, Moshi
UGONJWA wa kimeta (anthrax) umeua mtu mmoja na wengine 84 wakiendelea na matibabu huku 10 kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa ugonjwa huo umeibuka katika Wilaya ya Moshi Vijijini na umetokana na watu hao kula nyama ya ng'ombe anayesadikika kuwa na ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini, Annah Mwahalende alisema jana kuwa watu 84 walioshiriki kuchuna na kula nyama hiyo, walipata maambukizi ya ugonjwa huo.

“Taarifa hizi za ugonjwa wa kimeta zilithibitishwa na jopo la madaktari kutoka Hospitali ya Mawenzi ambako wagonjwa wanne kutoka katika Kijiji cha Kitandu wamelazwa wakiendelea na matibabu,” alisema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo alisema baada ya kupatikana kwa taarifa hiyo, wagonjwa walipatiwa matibabu na familia za wagonjwa hao 10 zimepatiwa dawa za kinga ya ugonjwa huo.

Mwahalende alisema halmashauri yake imeyafunga maduka mawili ya kuuzia nyama yaliyokuwa yakiuza nyama hiyo katika kijiji hicho.

Mkurugenzi huyo alisema timu ya wataalamu wa afya na mifugo wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa tarafa, kata na vijiji wametoa elimu ya ugonjwa huo kwa wananchi 500 hadi kufikia jana.

“Wagonjwa 10 waliripotiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi na ile ya Kibosho na wagonjwa wanne kati yao walilazwa lakini kwa bahati mbaya mmoja alifariki dunia” alisema.

Mwahalende alisema kutokana na kifo hicho, wataalamu hao wa afya walifuatilia na kusimamia mazishi ya aliyefariki pamoja na kutoa dawa za kinga kwa waathirika.

Taarifa juu ya ugonjwa huo ilipokewa kwa mara ya kwanza na mganga mkuu wa wilaya hiyo Februari 27 na uchunguzi ulifanyika na baadaye hatua za matibabu zilifuata.

Mkurugenzi huyo alisema halmashauri yake imejiwekea mikakati mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa huo ikiwamo kutoa elimu ya dalili na namna ugonjwa huo unavyoenezwa pamoja na kinga na tiba yake.

Alisema halmashauri hiyo itaendelea kuwafuatilia watu wote wanaohisiwa kula nyama hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa dawa pale inapohitajika na kubaini watu wengine watakaoonyesha dalili za kupatwa na ugonjwa huo.
Kimeta ni nini
Ni ugonjwa unawapata wanyama hususan wanaofugwa kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na wanaweza kumwambukiza binadamu.

Zamani watu waliokuwa wakiathirika zaidi walikuwa ni wafugaji, madaktari wa wanyama na wachuna ngozi.

Kuna aina mbalimbali za kuambukizwa ugonjwa wa kimeta lakini tatu ndizo zinafahamika zaidi. Aina ya kwanza ni ile ambayo mtu anaambukizwa kwa kuwa na kidonda, nyingine ni ya kuvuta hewa na ya tatu kwa kula nyama ya mnyama aliyeathirika.
Dalili za Kimeta

Dalili za kimeta hutofautiana kutegemea aina ya maambukizi, lakini kwa watu waliokula nyama ni-
- Maumivu ya tumbo
- Kuhara damu
- Kuharisha
- Homa
- Kuvimba midomo
- Kutapika na mara nyingine damu
Ni ugonjwa unaotibika kwa kutumia dawa za ‘antibiotics’ na mgonjwa anaweza kupona akiwahi matibabu.

Hakuna ushahidi juu ya mambukizi ya ugonjwa wa kimeta kutoka mtu kwenda kwa mtu mwingine na hata watu walio karibu na mgonjwa hawawezi kupewa dawa labda kama wameambukizwa na mnyama.
Chanzo.
Ugonjwa wa kimeta waua mmoja, 84 hoi
 
Anthrax: Images: Cutaneous Anthrax

Cutaneous Anthrax—Vesicle Development
Day 2


Day 4


Notice the edema and typical lesions
Eschar formation


Ulcer and vesicle ringBlack eschar, redness remains

Day 6

Left image: forearm lesion on Day 7—vesiculation and ulceration of initial macular or papular anthrax skin lesion.
Right image: eschar of the neck on Day 15, typical of the last day of lesion. From Binford CH, Connor DH, eds. pathology of tropical and extraordinary diseases. Vol 1. Washington DC: AFIP:1976:119. AFIP negative 71-1290-2
NEJM 1999:341:815-826


Day 10


 
Asante mkuu kwa tarifu nzuri Da ! Ugonjwa huu unamda mrefu umepotea tena umerudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…