Ugonjwa wa "kuamka huna hela mfukoni" na dalili zake.

Ugonjwa wa "kuamka huna hela mfukoni" na dalili zake.

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
👁️JINA LA UGONJWA
KUAMKA HUNA HELA MFUKONI.

👁️DALILI YA UGONJWA WA "KUAMKA HUNA HELA MFUKONI"
(a)
Mwili kuchoka na kukosa nguvu, ikiwemo kupoteza hamu ya kula.

(b) Kupoteza hamu na shauku ya kuwasiliana na watu au marafiki unaofanana nao kiuchumi. Unahisi kuwasiliana nao ni kuharibu salio lako.

(c) Kupata hamu ya kuwasiliana na marafiki au wadau wenye hela, na mara zote unajikuta unawaita majina ya ukuu (mfano: Bosi, mkuu, kiongozi, n.k)

(d) Hasira ndogo ndogo ambazo huja mara kwa mara, ikiwemo kuwachukia watu, marafiki, wafanyakazi, na wadau waliojipata kimaisha.

(e) Kuchukia pombe, mapenzi na mahusiano hasa mahusiano ya nje (kwa wenye ndoa). Wakati mwingine unakumbuka matukio ya starehe uliyotumia hela nyingi kizembe (mfano matukio yq kula bata) na kujiona ulikuwa mjinga wa kutoweka akiba ya hela.

(f) Kuuchukia mji au mkoa unapoishi. Mara zote unapatwa na hasira ya kuchukia mkoa au mji unapoishi na unatamani kuhama.

RIGHT MARKER
Dar es salaam.
 
Hii mada kuna watu inagusa maisha yao moja kwa moja kwa namna moja au nyingine. Katika hizo point lazima kuna mojawapo au zote itamgusa mtu. Ukiguswa confess!
 
Hii mada kuna watu inagusa maisha yao moja kwa moja kwa namna moja au nyingine. Katika hizo point lazima kuna mojawapo au zote itamgusa mtu. Ukiguswa confess!
Ndio maisha ni nauita UPEMI(Uhaba wa pesa mifukoni).
 
Ndio maisha ni nauita UPEMI(Uhaba wa pesa mifukoni).
hahahaaaa UPEM kuna wale huwa wakiona mambo ni magumu wanaenda kwa waganga afu mganga anakuambia kijana umelogwa naona kila unachofanya hakifanikiwi na alivo mjinga anatoa na ka akiba alikokuwa nako anampa mganga ili amsaidie apate pesa bila kuwaza kuwa mganga nae anatafuta pesa
 
Umepiga penyewe aisee 100%


Na ukipata unasahau shida zote..

Solution ni kufanya biashara hata ndogo ndogo Yani hela ushike shike..kuliko hizi za mara moja paah
 
Back
Top Bottom