Ugonjwa wa kusakata rhumba (kudance) ulioua watu huko Germany

Ugonjwa wa kusakata rhumba (kudance) ulioua watu huko Germany

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
dancing.jpg

Miaka zaidi ya 643 iliyopita, katika mji wa Aachen huko Ujerumani watu walianza kumiminika mitaani kutoka kwenye majumba yao na kuanza kusaka rhumba kwa kila aina ya staili. Wengine walicheza kiduku, wengine mapanga, wengine shaku shaku, wangine walishake, wengine wakacheza ngororo, ili mradi kila mtu alikuwa akisaka dance. Huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa mlipuko wa huu ugonjwa wa kusakata rhumba (dancing plague/choreomania). Ugonjwa huu ulisambaa katika bara la Ulaya kwa miaka kadhaa.

Mpaka leo hakuna ajuaye chanzo cha mlipuko huu. Wataalam na wanasayansi akiwemo Dr. Mwaka mpaka leo hawana majibu juu ya chanzo na sababu ya ugonjwa huu hataari. Watu walikuwa wakisakata rhumba pasipo kuwepo mziki wowote, na walikuwa wakicheza mpaka wanachoka wanakuwa hoi bin taaban lakini hawaachi wanaendelea kusakata rhumba mwanzo mwisho, yani kwa Kingereza ni 24/7. Yani ni kusakata dance utapumzika pale tu ukiishiwa nguvu na kuanguka ukafa.

Huko Ujerumani, mlipuko huu ulijulikana kama Rhumba la mtakatifu John au kwa Kiingereza St.John Dance (Kumbuka hili jina halina uhusiano na faru John au Mheshimiwa mkuu). Pia huu mlipuko ulikuwa si wa kwanza wala wa mwisho kutokea.

Watu walikuwa wakitengeza mzunguko wakashikana mikono, na ilionekana wazi kuwa walikuwa wamepoteza uwezo wa kuongoza viungo vyao. Walianza kusaka rhumba wakaruka kwa wehu mpaka waanguke chini kwa kuchoka kabisa. Pia walikuwa wakiunguruma na kutoa sauti kama vile wamekabwa. Wengine walikuwa wakianguka wakapumzika baadae wanaamka wakiwa salama salimini, kisha wanaanza tena kusakata rhumba.

Ugonjwa ulisambaa mpaka miji ya Liege, Tongres, Utrecht, na miji mingine kule Netherlands na Ubelgiji mpaka kwenye maeneo yaliyo wenye kingo za mti Rhine. Kwenye maeneo mengine ugonjwa ulijulikana kama St. Vitus' Dance. Sielewi kwanini hawa wajinga walikuwa wakiita gonjwa majina ya watakatifu wao.

Kanisa lilianza kudai ya kwamba gonjwa hili lilisababishwa na shetani ambapo shetani na lilidai wanaosaka rhumba kwa kuugua gonjwa hili wameingiliwa na shetani au wamelaaniwa na watakatifu. Kule Italia gonjwa hili lilijulikana kama Tarantism huku ikiaminika kwamba gonjwa hili lilisababishwa na kung'atwa na buibui.

Wataalam wa sasa baadhi yao siyo wote maana hata mimi nimekataaa sijakubaliana nao, wanadai kwamba gonjwa hili lilisababishwa na aina fulani ya fingus ambayo ilisababisha watu kupata wenge na kushindwa kuongoza misuli na maungo yao.

Sasa kama wewe ni mpenzi wa kudance sana huenda una chembechembe za hili gonjwa. Mbaki salama
 
Tuletee hizi story za Killer Crown'killer Doll
 
Daudi alipocheza hadi kanzu ikamvuka alikua na huu ugonjwa pia?
Daudi hakufa mkuu, halafu ilikuwa inapigwa vifaa yani kulikuwa na ala na kuimba, hawa walikuwa wanadance bila hata kusikia chochote mkuu.
 
Hahahhaa imebidi tucheze tuu hakuna namna. Usipochza huli
 
Back
Top Bottom