Habari ndugu!!!....kuna huu ugonjwa maarufu sana hapa jijiji dar,ugonjwa wa macho,red eyes...unaofanya macho kuwasha na kuuma na kuwa mekundu sana na kuvimba..ni nini chanzo chake na namna ya kujikinga usikupate
Wanafunzi DUCE wakumbwa na ugonjwa wa Macho Mekundu (Red Eyes)
JICHO ni moja ya kiungo muhimu katika mwili wa binadamu, ugonjwa wa macho mekundu, maarufu kama 'Red Eyes' ni moja ya magonjwa ya muda mrefu na imekuwa ni hali ya kawaida ya kila mwaka wakazi wa maeneo mbalimbali kukumbwa na ugonjwa huo hususani wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
Maeneo ya jirani na vilipo vyuo hivyo wananchi wanakumbwa na ugonjwa huo, huku wagonjwa mbalimbali wakiripotiwa kuugua ugonjwa huo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).
FikraPevu imeshuhudia wengi wa wagonjwa wakiwa katika hali ya awali ya ukuaji wa ugonjwa huo na macho yao yameonekana kuwa mekundu na kuvimba kama ilivyo kawaida ya ugonjwa huo katika dalili zake za awali.
Mmoja wa wauguzi katika Zahanati ya Chuo hicho (hakupenda jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji) alisema hadi Januari 20, 2014 idadi ya wagonjwa waliofika katika Zahanati hiyo kupatiwa matibabu ilikuwa ni wanafunzi 700 (idadi hii inaongezeka kila siku) na wengine hawaendi katika Zahanati hiyo kutibiwa (wanaenda kutibiwa nje ya Zahanati hiyo).
Baadhi ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huo walionekana kuvaa miwani myeusi kusitiri macho yao mbele za watu, na kwamba ugonjwa huo ulianza tangu wiki moja iliyopita.
Amiri Juma, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo amesema pamoja na serikali kujitahidi kutoa fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu zamu hii hali imekuwa tafauti kwa utoaji wa huduma hiyo kwani hali ni ngumu kwa wanafunzi wanaotegemea fedha hizo boom.
Ugonjwa wa 'Red Eyes'
Ugonjwa wa macho mekundu kwa kawaida unasababishwa na kitu kinachoitwa tabaka la juu ya jicho hali ambayo inatakiwa ilifanye jicho kuwa jeupe na linapobadilika na kuwa jekundu hapo ndipo binadamu anapotakiwa kujua kuwa tabaka jeupe linaleta chakula na hewa kwa ujumla wake. Pia vipo vimishipa kwenye macho ambavyo vinapovimba husababisha ugonjwa wa Red Eyes.
Hadi sasa chanzo halisi cha ugonjwa huo hakijajulikana kuwa unatokana na nini lakini tafiti zinaonyesha kuwa vipo viashilia vinavyoonyesha kuwa ugonjwa huo unatokana na kuwepo kwa michirizi inayokatiza kwenye jicho ambayo huathirika mfumo wa damu.
Sababu ya jicho kuvimba inatokana na vumbi, mzio/aleji na inaweza kuwa moshi, unywaji wa pombe, kuchelewa kulala na mwingine anaweza kukumbana na hali ya mishipa kujikunja hali inayopelekea mishipa kushindwa kusambaza damu kama kawaida.
Daktari Erick Matimbwi, mtaalamu wa tiba mbadala jijini Dar es Salaam, anasema sababu nyingine ya ugonjwa huo ni kuwa na ugonjwa wa Shinikizo la damu la juu na ukosefu wa vitamin A. B3 au B6 na kwamba idadi kubwa ya watu wanaweza kuambukizwa ugonjwa huo kwa wakati mmoja katika baadhi ya nchi za Afrika.
Utumiaji wa vitamin A, B, B6 na nyingine chachu zitokanazo na vitamin za mboga za majani, matunda kwa wingi vinasaidia kuweka kinga ya kuugua ugonjwa huo pamoja na kula maharage kwa wingi kwani inasababisha vitamini B.
Moja ya sababu inayotajwa kusababisha hai hiyo ni neon la kitaalamu lijulikanalo kama chavua katika anga hewa licha ya asili ya macho kuwa na uzio wa kuzuia kitu isichopata na acho kukizuia ili kisiingie ndani.
Aidha, imeelezwa kuwa ugonjwa huo unasababishwa na aina mbalimbali za bacteria. Watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea kwa kawaida mamcho yaop huwa mekundu kuliko vijana.
Tafiti zinaonyesha kuwa macho ya mwanadamu hayatakiwi yazidi kuwa mekundu na watu waliochini ya umri huo wanatakiwa kuwa makini wanapoona macho kuwa mekundu wazingatie kwende kwa madaktari kujua chanzo na tiba.
Mgonjwa anapohitaji tiba anatakiwa kutumia njia ya kumuona mtabibu haraka iwezekanavyo ili kujua kama jicho lina bacteria au limeathiriwa na mwanga mkali ambao pia unasababisha ugonjwa wa mamcho kuvimba na kwamba uvaaji wa miwani meusi inaweza kusababisha mikunjo ya mishipa ya damu.
Copy: Wanafunzi DUCE wakumbwa na ugonjwa wa Macho Mekundu (Red Eyes)