JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Marburg ni nini?
Kwa mujibu wa WHO, virusi vya marburg ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 29 kuambukizwa na saba kati yao kufariki dunia mwaka 1967 huko Marburg na Frankfurt, Ujerumani pamoja na Belgrade huko Serbia.
Hata hivyo, WHO walisema virusi vya marburg vilipatikana kwa mara ya kwanza kwa tumbili wa kijani kibichi wa Kiafrika.
Miongoni mwa dalili za ugonjwa huo ni kikohozi, kuhara, maumivu ya viungo na kutapika na mara nyingi hata upungufu wa damu katika mwili.
Imeelezwa hata watu wakipona, damu au shahawa zao zinaweza kuwaambukiza wengine kwa miezi mingi baadaye.
Ugonjwa unavyoambukiza
Juzi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema marburg huambukizwa kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine hususan kwa njia ya kugusa majimaji, mfano mate, mkojo, damu, machozi au kinyesi kutoka kwa maiti au mgonjwa mwenye dalili.
Alisema maambukizi yanaweza kutokea pia kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu, iwapo mtu atakula au kugusa mizoga au wanyama walioambukizwa.
Alitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni homa, kuumwa na kichwa, maumivu ya misuli, kuishiwa nguvu, kutapika na kuharisha, kutoka damu sehemu za wazi za mwili na nyingine zifananazo na hizo.
“Ugonjwa huu hauna tiba mahususi isipokuwa hutibiwa kwa dalili anazokuwa nazo mgonjwa,” alisema.
Waziri Ummy alitoa wito kwa watumishi wa afya nchini wakati wote wa kutoa huduma kwa wananchi wawe makini, ili kuzuia maambukizi kutoka kwa wagonjwa.
“Nichukue fursa hii kuwatoa hofu kuwa hadi sasa Serikali imefanikiwa kudhibiti kasi ya maambukizi mapya ya ugonjwa huu na tutaendelea mpaka siku 21 tusipobaini mgonjwa mpya tutatoa taarifa za kuutokomeza kabisa,” alisema.
Virusi vya Marburg vilipatikana kwa mara ya kwanza kwa tumbili wa kijani kibichi wa Kiafrika
Jinsi ya kudhibiti
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa linalozalisha chanjo duniani Gavi, watu barani Afrika wanapaswa kuepuka kula au kushika nyama ya porini.
Hata hivyo, WHO wanasema watu wanapaswa kuepuka kuwa karibu na nguruwe katika maeneo yenye mlipuko.
“Wanaume ambao wamekuwa na virusi wanapaswa kutumia kondomu kwa mwaka mmoja baada ya kupata maambukizi au hadi shahawa zao zitakapothibitishwa mara mbili kuwa hazina virusi vya ugonjwa huo.
“Na wale wanaozika watu waliokufa kutokana na virusi vya ugonjwa huo wanapaswa kuepuka kugusa mwili,” waliainisha WHO.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu alisema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo na tayari wameshachukua hatua za udhibiti.
Alisema mtu yeyote mwenye dalili za homa, kutapika, kuharisha, kutoka damu na mwili kuishiwa nguvu anashauriwa kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya mapema kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Profesa Nagu alisema ni muhimu kutoa taarifa mapema kwenye kituo cha kutolea huduma kilicho karibu au kupiga simu namba 199 bila malipo endapo utamuona au kukutana na mtu mwenye dalili kama hizo.
“Kuepuka kumgusa mgonjwa au majimaji ya mwili mfano mate, machozi, damu, mkojo na kinyesi yatokayo kwa mgonjwa au mtu yeyote mwenye dalili hizo,” alisema.
Alibainisha iwapo itamlazimu kumhudumia mgonjwa kwa dharura ni muhimu kuchukua tahadhari ya kujikinga na majimaji yoyote kabla ya kumhudumia.
“Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono, ili kujikinga na magonjwa yote ya kuambukiza.
“Kwa sasa ni muhimu kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono, kushirikisha wataalamu wa afya katika shughuli za misiba na mazishi katika kipindi hiki, lakini pia watumishi wa afya wazingatie kanuni za kujikinga na magonjwa ya kuambukiza,” alisema Profesa Nagu.
Chanzo: Mwananchi
=====================================
Ugonjwa wa Marburg ni nini?
Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt. Ujerumani na Belgrade huko Serbia.
Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kikohozi, maumivu ya viungo, kuhara na kutapika, na mara nyingi hata upungufu wa damu katika mwili.
Mlipuko huo ulitokana na tumbili wa Kiafrika walioagizwa kutoka Uganda. Lakini virusi hivyo vimehusishwa na wanyama wengine tangu wakati huo.
Na miongoni mwa wanadamu, huenezwa zaidi na watu ambao wamekaa kwa muda mrefu katika mapango na migodi iliyo na popo.
Huu ni mlipuko wa kwanza nchini Ghana - lakini nchi kadhaa za Afrikazimewahi kuripoti mlipiko wa virusi ikiwa ni pamoja:
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
Kenya
Afrika Kusini
Uganda
Zimbabwe
Mlipuko wa mwaka 2005 nchini Angola ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 300. Lakini barani Ulaya, ni mtu mmoja tu amefariki katika kipindi cha miaka 40 - na mmoja nchini Marekani,baada ya kurejea kutoka katika safari ya kuzuru mapango nchini Uganda.
Milipuko mikubwa:
2017, Uganda: visa vitatu, watu watatu walifariki
2012, Uganda: vis 15, watu wanne walifariki
2005, Angola: visa 374, watu 329 walifariki
1998-2000, DR Congo: visa 154 cases, watu 128 walifariki
1967, Ujerumani: visa 29, watu saba walifariki
Chanzo: WHO
Inasababisha ugonjwa gani?
Unaanza ghafla na:
Homa
Kuumwa vibaya na kichwa
Kuumwa na misuli
Hii mara nyingi siku tatu hufuatwa na:
Kuharisha
Kuumwa na tumbo
Kichefuchefu
Kutapika
WHO inasema: "Mwonekano wa wagonjwa katika awamu hii umeelezewa kuwa unaonyesha sifa za 'kama mzimu', macho ya ndani, nyuso zisizo na hisia na uchovu mwingi."
Baadhi ya watu hutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili na kufa siku nane hadi tisa baada ya kuugua kwa sababu ya kupoteza damu nyingi na mshtuko.
Kwa wastani, virusi huua nusu ya walioambukizwa, WHO inasema, lakini aina hatari zaidi imeua hadi 88%.
Je, inaeneaje?
Popo wa matunda wa rousette wa Misri ndiye mbebaji mkuu wa virusi
Popo wa matunda aina ya rousette wa Misri mara nyingi huwa na virusi. Nyani wa kijani kibichi na nguruwe wanaweza pia kubeba.
Miongoni mwa wanadamu, huenea kupitia maji ya mwili na malazi yaliyochafuliwa nao.
Na hata watu wakipona, damu au shahawa zao, kwa mfano, zinaweza kuwaambukiza wengine kwa miezi mingi baadaye.
Je, inaweza kutibiwaje?
Hakuna chanjo maalum au matibabu ya virusi.
Lakini aina mbalimbali za bidhaa za damu, madawa ya kulevya na matibabu ya kinga yanatengenezwa, WHO inasema.
Na madaktari wanaweza kupunguza dalili kwa kuwapa wagonjwa waliofika hospitali maji mengi ili kuchukua nafasi ya damu iliyopotea.
Vinawezaje kudhibitiwa?
Watu barani Afrika wanapaswa kuepuka kula au kushika nyama ya porini, Gavi, shirika la kimataifa linalokuza upatikanaji wa chanjo, linasema.
Watu pia wanapaswa kuepuka kuwa karibu na nguruwe katika maeneo yenye mlipuko, WHO inasema.
Wanaume ambao wamekuwa na virusi wanapaswa kutumia kondomu kwa mwaka mmoja baada ya kupata alili au hadi shahawa zao zitakapothibitishwa mara mbili kuwa hazina virusi.
Na wale wanaozika watu ambao wamekufa kutokana na virusi wanapaswa kuepuka kugusa mwili.
Chanzo: BBC