Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,855
- 189,385
MINAMATA DISEASE
Ugonjwa uliogundulika kwa mara ya kwanza sehemu iliyoitwa Minamata kwenye mji wa Kumamoto huko Japan mwaka 1956.
Nini chanzo za ugonjwa wa Minamata?
Tarehe 21 april mwaka 1956, Mtoto wa kike wa umri wa miaka 5 alichunguzwa katika hospitali ya shirika moja la Chisso huko Minamata. Madkatari walichanganywa na dalili za mtoto huyo:baadhi ni kushindwa kutembea, kuongea pia alikuwa akishtuka shtuka kila baada ya muda fulani(Convulsions).
Baada ya siku mbili kupita dada yake na mtoto huyo pia alianza kuonesha dalili zile zile, mama wa watoto hao aliwaambia madaktari mtoto wa jirani yake pia alikuwa ana matatizo kama ya mwanae. Ufanyika uchunguzi wa nyumba kwa nyumba wagonjwa takribani 8 zaidi waligundulika na kupelekwa hospitali.
May Mosi ya mwaka huo huo mkurugenzi wa hospital hiyo (Chisso) aliripoti kwa mamlaka zote za afya kuwepo kwa janga la ugonjwa usiofahamika wa mishipa ya fahamu na kupewa jina la Minamata.
Serikali pamoja na watendaji wa afya mbalimbali waliunda kamati iliyoitwa “The Strange Countermeasures Committee” mnamo mwishoni mwa mwezi May 1956. Mwanzoni walidhani ni ugonjwa wa kuambukiza hivyo hatua kama ya kutengwa kwa wagonjwa sehemu maalumu zilichukuliwa haraka ila chakushangaza zaidi wagonjwa ndio kwanza waliendelea kuongezeka idadi kila kukicha.
Wakati tafiti mbalimbali zikiendelea kufanyika kufahamu nini chanzo chake, wataalamu walikutana na mambo ya kushangaza zaidi ambayo ni tabia zilizokuwa zinaoneshwa na paka pamoja na wanyama waliokuwa karibu na maeneo ya nyumba za walioathirika na ugonjwa huo
Ilithibitika kuanzia mwaka 1950, Paka walionekana wakipata dalili za kushtuka shtuka, kuwa vichaa na baadae kufa. Watu wa eneo hilo la Minamata wakaupa ugonjwa huo wa Paka jina la “Cat Dancing Fever”
Pia Kunguru na ndege wa aina tofauti tofauti maeneo hayo walikuwa wakianguka na kufa, magugu maji pia yalikuwa hayastawi kama ilivyozoeleka pembezoni mwa bahari bali yaliendelea kunyauka kwa kasi.
Madhara yaliongezeka na idadi ya watu iliongezeka, kamati ya mwanzo iliomba msaada zaidi ya watafiti kutoka chuo kikuu cha Kumamoto.
August 24,1956 kikundi cha watafiti kutoka chuo kikuu cha Kumamoto kiliundwa. Wagonjwa walilalamika kwa kuanza kupoteza uwezo wa kuhisi,kupata ganzi miguuni na mikoni. Kuliambatana na kushindwa kutembea au kukimbia, pia sauti zao zilianza kubadirika kuwa nyembamba. Wagonjwa wengi walisema uwezo wa kuona, kusikia na kumeza umepungua. Kwa ujumla baada ya dalili zote hizo vilifuata vifo.
October 1956, wagonjwa 40 waligundulika kati yao 14 walifariki dunia.
Ulikuja kufahamika sababu ilikuwa ni madini ya zebaki(Mercury) yaliyokuwa yakimwaga kama maji taka na shirika moja la uzalishazi wa chemikali lililoitwa Chisso ambalo lilianza mwaka 1908.
Tutaendelea.

- Namna ulivyogundulika?
- Athari za Minamata ambazo zimedumu kwa muda wa nusu karne.
- Fidia kwa wahanga wa ugonjwa wa Minamata.