Ugonjwa wa P.I.D kwa mwenza

sam green

Senior Member
Joined
Feb 21, 2020
Posts
184
Reaction score
274
Habari wana JF.

Poleni na majukumu, naomba msaada kuhusu ugonjwa wa PID. Mimi nina mpenzi wangu wiki iliyopita tulikutana kimwili.

Kawaida tu, lakini kuna nyakati siku mbili baadaye nikaona mabadiliko kwangu, moja ni kuwashwa sana kwenye kichwa cha uume na nina hisia ya kutaka kujikuna muda wote. Pia, kuna vipele vidogo vidogo vimejitokeza kwenye kichwa cha uume.

Nikakaa kimya nikijua ni hali tu sasa, lakini yeye ndiyo kanambia anaumwa PID. Anatokwa na majimaji meupe na harufu mbaya ukeni.

Nikajaribu kuangalia, inatokana na nini? Nikaona asilimia kubwa inatokana na kujamiana na mtu mwenye maambukizo.

Lakini nimekuja kwenu naomba kujua huu ugonjwa unatokana na nini sana? Mimi sijawahi kulala na mwanamke mwingine zaidi ya yake katika kipindi changu chote cha miaka minne nipo naye. Sijawahi jaribu kumsaliti hata sekunde.

Naomba mniambie inatokana na nini? Je, alikutana na mwanaume mwenye maambukizo, yaani alinisaliti au imekuwaje hapa? Maana sielewi, naomba majibu, ndugu zangu.
 
Sio kwakujamiiana tu....kwa sisi wanawake inatokana na aina ya pedi tunazotumia sasa ndio imekua chanzo kikuu....na mwanamke anapofua chupi kuanika ndani nayo inasababisha sana usije ukamuacha mwenzi wako bure ukizan anakusaliti
 
Sio kila PID inatokana na magonjwa ya zinaa wakati mwingine ni bakteria wa kawaida wanaenda kushambulia mlango wa kizazi na mirija, pengine mwanamke ana tabia ya kujisafisha kwa vidole ukeni, kujitia manukato, Uti ya mara kwa mara, uzazi wa mpango, pedi zenye kemikali, usafishwaji mbaya kwenye utoaji mimba, n.k

Mwanamke hawezi kumuambukiza mwanaume PID ila mwanaume anaweza akampa virus, fungus, bakteria mwanamke na kumpelekea akapata PID,

Nendeni nyote kituo cha afya mkapime.
 
Sio kwakujamiiana tu
Bacterial infection kupitia hizo njia zingine ni kiwango kidogo sana BUT mostly ni STIs.

Vijana wa kiume tumieni Kinga. hasa nyie ambao mnakutana na wapenzi wenu baada ya kipindi kirefu kidogo.

Ninawatibu sana Mabinti wa miaka kati ya 20 - 27, na chanzo kikubwa huwa ni STIs.
 

Mkuu!
Msaada hapo, nina mwenza wangu yupo mkoa jirani na nilipo ila ana changamoto iliyoelezewa hapo tulishashauriana apate matibabu kabla hatujaonana kwakua tulikua na mpango wa kupata familia, sasa katika hali hiyo Mimi nilisema siwezi kukutana nae kabla hajapona.
Ameshatumia dawa nyingi za huko hospital ila ni kama hazijamsaidia hv, aidha amechomwa sindano na kutumia dose mpk mwezi mzima lakini hajafanikiwa.
Tatizo lilianza mwaka 2019 baada ya kupata miscarriage.
 
Duh hali ni mbaya aaseee
 


Jitibu, kaa pale naye sasa!
 
Mkuu kama mwenza wako hajapona hayo maradhi ya PID nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kumtibia maradhi yake apate kupona .
 
Uti isiyotibika
Magonjwa ya zinaaa yanayotibiwa nusu nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…