Penologist
JF-Expert Member
- Feb 25, 2019
- 790
- 1,923
Shukran mkuu.Pole Sana Kwa Kuumwa
Kuwa makini.... shauri yako....
Vinatoa usaha au maji?Hapa sio vishilingi ni vipele kikipona kimoja kinatokea kingine pia huwasha sana kuna wakati vinakuwa vikubwa kama majipu.
Nimepoteza mawasiliano naye baada ya kuondoka morogoro.Je umejaribu wasiliana na huyo binti baada ya kupata huo ugonjwa
Amani iwe nanyi wakuu.
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu.Ugonjwa juu usiokuwa na jina la kitaalamu umenisumbua kwa mwaka sasa.Niliambukizwa nilipofika morogoro kufanya research.Baada ya kumaliza shuhuli zangu nilifika mzumbe mtaa wa changarawe na kukaa kwa miezi miwili nikiandaa report.Hapo ndipo nilipo kutana na binti mmoja sikulaza damu nikamtongoza akanielewa akaanza kuwa anakuja kwangu nilipopanga.Kabla hatujakutana kimwili alipendekeza tukapime kituo cha karibu hapohapo mzumbe tukapima HIV wote tuko negative.
Baada ya kurejea kwangu tulikutana kimwili.Ila tulipo kutana Sikh iliyo fwata akaniambia P ntakuambukiza tangatanga nika muuliza ndio nini akanionyesha vidoti vidogo kama nukta za makerpen mgongoni.Ila sikuona tatizo nikampeleka kwangu tukalala usiku bila kukutana kimwi niligunduna kua ana jikuna sana usiku.Ndipo nilipo amua kuachana nae.
Week moja ilipopita nilianza kupata muwasho mkali sana mwilimzima.Kila ifikapo asubui na usiku nilikuwa nawashwa sana.Baadae nikapata vipele kwapani mapajani kwenye makalio na kwenye viganja vya mikono.Nilipo ends hospital ya mzumbe kupima sikukutwa na ugonjwa wowote wa ngono wala wa ngozi.Hivyo nikaandikiwa gentrisone cream kwa muda.Iyo hali ya kuwasha haikuisha vipele viliendelea kutoka hadi kwenye uume ila havitoi fluid na muda mwingine vinawasha sana.Kila nikienda hospital napimwa naambiwa sinaugonjwa wowote.Kwa docter wa ngozi ananipa cream na vidonge ila ndio vinazidisha.
Nimetumia dawa za asili lakini bado vipele vinatokea tena nikienda kwenye mikoa ya baridi vinakuwa kama majipu.
Wenyeji wa morogoro hasa waluguru naomba mniambie ugonjwa wa tangatanga ni ugonjwa unaosababishwa na nini naunatibiwa na dawa gani ya asili kwa kua yule mwanamke aliniambia ameambukizwa na dadayake pia ametibiwa na ndugu zake ndio maana yeye hana vipele wala majipu.Wakuu nisaidieni kwa kuwa nateseka sana natamani atakufanya suicide au murdering kwa uyo mwanamke ila imani yangu inanifariji.Ahsanteni.
Sawa mkuu.cheng hahahaha ngoja nimuulize jamaa yangu wa huko kama anafahamu dawa
Wanaoenda kaumba ndio hao wa changarawe.Vp mkuu unajua chochote kuhusu tangatanga?.
Nilifika kaloleni doc wa ngozi alinipima hadi fluid hakuna chochote alicho nipa zaidi ya gentrisone cream ethromycine.Baada kumaliza dose nilirudi akaniongezea ethro lakini hazikusaidia.Sasa mbona huoneshi kama umefanya juhudi za kutosha kwenda hsptl? Kama dokta alikupa cream, haijasaidia, si uende mbali zaidi? Umemuona bingwa wa ngozi?
Kuhusu ugonjwa sijui kwanini unauliza sasa, ushaambiwa ni Tangatanga, na wewe ulitangatanga, sasa unauliza nini tena hapo? Ndiyo faida za kutanga huko!
Ahsante mkuu nitazingatia maelekezo yako.Me mwenyeji wa Moro naujua huo ugonjwa rafiki zangu wengi wameugua wakati tunasoma. Ni ugonjwa wa ngozi ambao ni vigumu kupona haraka ila ukiwa na nia utapona tena kwa dawa nyepesi sana.
Nenda duka la dawa nunua dawa ya kupaka inaitwa Whitefield ipo kama mafuta ya mgando hivi. Hii ndo kiboko ya fangasi ya ngozi. Ukiipata hii dawa ni hatua moja ila unatakiwa ufuate maelekezo jinsi ya kuitumia ili upone maana wengi hufeli hapa.
Hakikisha unaoga angalau mara mbili kwa siku na asubuhi na jioni au usiku. Baada ya kuoga usipake mafuta yoyote ila paka hiyo Whitefield mwili mzima kuanzia kichwani hadi unyayoni ila kuwa makini kwenye sehemu laini kama mapumbu maana inawasha baadhi ya sehemu laini kama ikulu huko.
Pia hakikisha ukivaa nguo usiirudie tena mpaka ifuliwe na kupigwa pasi tena ikiwezekana fua kwa jik na sabuni ili kuondoa fungus. Na kitandani shuka ukilalia mara moja itoe uifue kifupi inabidi umaintain usafi kwa hali ya juu sana.
Tumia hiyo dawa kwa wiki mbili mfululizo utaoma matokeo. Pia kama unawashwa sana basi tafuta vidonge vinaitwa cetrizine vinasaidia kuondoa muwasho kwenye ngozi. Ukienda duka la dawa utaelekezwa matumizi ya hivyo vidonge.
So vitu vitatu muhimu
1. Tumia Whitefield kupaka mara mbili kwa siku 2. Maintain usafi, nguo utakayotumia usiirudie hata iwe leso.
3.Tumia cetrizine kuondoa muwasho.
Hiyo ndiyo dawa ya utangatanga nimekushauri nikiwa mkazi wa Moro so naujua huo ugonjwa pia nimekushauri kama mtaalam wa afya by professional. Huo ugonjwa hospital utapata shida kupona.
Sent using Jamii Forums mobile app
Je, hivyo vipele ukivitoboa ile sehemu inabaki na kovu ambalo ngozi yake inakuwa nyembamba na inabanduka? Hilo jina la ugonjwa silijui ila kwa maelezo yako yanaenda na ugonjwa kama huo ambao kwa dawa za asili unapona kabisa yani huwezi amini. Mimi sio daktari ila naweza kukuelekeza sehemu ya kupata hiyo dawa tena gharama ni ndogo mno kiasi kwamba unaweza usiamini lakini tatizo linaisha kabisa.Nilifika kaloleni doc wa ngozi alinipima hadi fluid hakuna chochote alicho nipa zaidi ya gentrisone cream ethromycine.Baada kumaliza dose nilirudi akaniongezea ethro lakini hazikusaidia.
Karibu mkuu elezea hiyo dawa hapahapa itawasaidia hata na watu wengine.Je, hivyo vipele ukivitoboa ile sehemu inabaki na kovu ambalo ngozi yake inakuwa nyembamba na inabanduka? Hilo jina la ugonjwa silijui ila kwa maelezo yako yanaenda na ugonjwa kama huo ambao kwa dawa za asili unapona kabisa yani huwezi amini. Mimi sio daktari ila naweza kukuelekeza sehemu ya kupata hiyo dawa tena gharama ni ndogo mno kiasi kwamba unaweza usiamini lakini tatizo linaisha kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app