achengula
JF-Expert Member
- Jul 30, 2009
- 369
- 62
Ukurutu(mange) ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukizwa wenye dalili kuu zifuatazo: ngozi kuwa ngumu yenye magaga, ngozi kuwasha sana na kupotea kwa nywele/au manyoya unaosababishwa na wadudu wadogo sana wanaoingia na kukaa ndani ya ngozi. Wadudu hawa wanajulikana kama mange mites, lakini kuna aina tofauti zinazosababisha ugonjwa huu kulinga na aina ya mfugo mdudu anaoshambulia. Mwanadamu pia anaweza kuupata ugonjwa huu na ipo aina moja ya menji inayoweza kumshambulia mwanadamu inayoitwa kitaalamu Sarcoptes scabiei. Kwa daalili na jinsi ya kupambana nao pamoja na mambo yahusuyo mifugo na ufugaji soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA