Ugonjwa wa wadudu kula uti wa mgongo na ubongo

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Posts
2,659
Reaction score
2,827
Wadau habarini,naomba kujua kwa wataalamu au wenye kujua hasa,ugonjwa tajwa hapo juu unasababishwa na nini na madhara yake ni yapi,natanguliza shukrani
 
Reactions: RR
Ebu fafanua vizuri wadudu wanao kula uti wa mgongo una maanisha nn au ulitaka kusema nn hapo? Pangilia swal vizuri au una maanisha MENINGITIS.?? TAXOPLASMA GONDII??? CRYPTOCCOCCUS MENINGITIS..?? MENINGOCOCCOS..??
Jaribu kuangalia izo uone swali lako limelenga wapi kati ya hizo inflamation..??
 
mkuu,kiufupi ni hivi,nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye hivi karibuni alifariki dunia,sasa nilipouliza chanzo hasa kilichopelekea kif chke nikaambia alikuwa kitandani kwa wiki mbili nyuma kabla ya kifo chake akihangaika na ugonjwa huo yani wadudu kuingia kwenye uti wa mgongo na kutafuna ubongo,ndio maana nikataka kujua huu ni ugonjwa gani coz jamaa alikua rafiki yangu mkubwa sana na kifo chake hata leo nasononeka
 
Sawa mkuu ila kwakuwa hauja taja dalili wala kiashiria chchte chaku onyesha ni ugonjwa gani kati ya hayo hapo juu inakuwa ngumu kuku elewesha. Lakini common huwa ni cryptoccocus Meningitis. Huu ugonjwa huenezwa na fungal aina ya cryptoccocus hushambulia uti wa mgongo na mfumo mzima kwa ujumla.
Transmtion: huambukizwa kwanjia ya hewa pia kwanjia ya vumbi sana sana. Pia huwapata watu ambao kinga zao za mwili zimeshuka sana sana HIV +ve.
Dalili kubwa ya huu ugonjwa ni homa, maumivu makali ya uti wa mgongo, dalili kubwa ya huu ugonjwa ni
stiff neck shingo inakuwa ina kakamaha mgonjwa ana shindwa gusisha kidevu kwenye kifua.
Diagnosis yake ni CSF(
celebral spinal fluid) hii fluid huvutwa kwnye lumber pingili za uti wa mgongo... ni moja kati ya specimen collection inayo uma sana hosptal nafikir kuliko zote.
Hii homa ya uti wa mgongo ina sababisha vifo vingi vya haraka kama mtu hajapata matibabu kwa u haraka.
Nkipata mda nita ya elezea hayo mengine alafu ww uta unganisha dot.....
 
Aseeh!! ilinibidi nigusishe kidevu kifua!!..
 
dah,mkuu asante sana kwa kunijuza hayo,walau sasa naweza kupata mwanga halisi juu ya kile chenye kilichoweza kumuangamiza jamaa yangu,sijataja dalili coz wik nnei nyuma kabla hajafariki nilipokutana naye alikuwa yuko powa kwa kumuangalia,coz tulistorika mengi sana ya kimaisha,then toka hapo sikuwa na mawasilian naye zaid y kuja kupata taarifa za kifo chake.

nakumbuka niliwahi kuuliza watu wengine wa nnje ya jf kila mtu akawa na jibu lake lakini main jibu wakanijibu kuwa gonjwa hilo linahusianishwa na mambo ya kishoga,yani mtu mwenye kuingiliwa mara kwa mara sasa madhara yake ni shahawa zile kuingia kwenye uti wa mgongo na kuzalisha bacteria wanaokula hadi ubongo.

nilipopata jibu hilo sikuridhika nalo hasa coz nilikuwa namjua fika huyu jamaa yangu vema sasa nikawa nimepatwa na mshangao juu ya sababu za ugonjwa huo na maisha yake,(japo inawezekana alikuwa anafanya kisiri,hilo sina uhakika kwa kuwa sikuwa nipo naye kila siku) lakini kimuonekano hakuwa na viashiria vya kunifanya niamini kuwa jamaa alikuwa punga..
 
Mkuu hizo ni imani potofu...sidhani kama kuna ugojwa wowote wa uti wa mgongo unao husiana na ushoga ...
 
Mkuu hizo ni imani potofu...sidhani kama kuna ugojwa wowote wa uti wa mgongo unao husiana na ushoga ...
ndiyo maana nikaja hapa jf kujua zaidi,maana binafsi nilianza kukosa furaha na uzuni yangu ikaongezeka maradufu
 
Ila huu ugonjwa wengi c rahisi kumpata mtu wa kawaida mala nyingi huwapata watu wenye HIV coz kinga zao zinakua ndogo saana ila otherwise mwili unaweza kuzuia fresh nakumbuka banza stone pia huu ugonjwa ndio uliomuondoa dunian pia kuna bro kigogo pale nae huu ugonjwa umemuondoa ko mara nyingi HIV positive wako katika hatari kubwa sana ya kushambuliwa na hu ugonjwa
 
doh,so kumbe inawezekana hata huyu jamaa yangu alikuwa ameathirika siyo?
 
Hakuna ukwel wowote hapo maana mara nyingi hao fangasi wanakuwa ni opportunistic disease kwa watu wenye HIV +ve lakin ata watu wa kawaida upata japo kwa shida... pia kama ni taxoplasma pia nao ni nyemelezi... hivyo hakna lolote linalo husiana na mapenzi hapo. Wala ushoga. Wa bongo ni watu wakusema ovyo.
 
Hhakuna ushaidi hapo. Hiyo ni homa ya uti wa mgongo ni kama homa zingine tu.
Sawa mkuu ushahidi haupo ila kwa kawaida huo ugonjwa n ngumu kumpata mtu mwenye kinga nzuri ya mwili datc why wanahusianisha sana na ukimwi..........
 
kumbuka kuna bacterial meningitis , ambayo sio HIV opportunistic infection. Inapiga mtu yeyote.
doh,so kumbe inawezekana hata huyu jamaa yangu alikuwa ameathirika siyo?
huenda ikawa hivyo lakini pia huenda ikawa sivyo.
Wapo bacteria wanaosababisha ugonjwa kama huo ambao hawajali cha ukimwi wala nini, ilimradi tu ukiwapata na wakafika kwenye uti wa mgongo basi wanafanya yao..., na mgonjwa asipokuwa mahali anapoweza kutibiwa kwa haraka anaweza kupoteza maisha ndani ya siku chache tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…