Ugumu katika maisha/biashara

Ugumu katika maisha/biashara

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
DEPRESSION / TROUGH

Hii ni stage katika maisha, biashara ambayo mambo huwa magumu sana na ugumu huja kuathiri uchumi wa dunia nzima.

Hiki ni kile kipindi ambacho mtu hukata tamaa na kupoteza matuaini kabisa kuhus maisha na kujiona hana umuhimu wa kuendelea kushi.

Hiki ndio kipindi ambacho watu wengi hutamani kufa, hukimbia familia, na wengine kujinyonga.

Mfano:

Mwenye kiwanda hukosa mauzo ya bidhaa anazozalisha, kwahiyo anajikuta

- hawezi kulipa kodi ya jengo

- hawezi kulipa kodi ya serikali

- hawezi kulipa mishahara ya wafanya kazi

- hawezi kuwasomesha watoto wake shule nzuri

Kwahiyo anaamua kufunga kiwanda chake, kitendo cha huyu mfanyabiashara kufunga kiwanda chake basi ndio jinsi depression inavyozidi kuambukizwa kwa watu wengine.


Mfano:

Waliokosa ajira kutokana na kufungwa kwa kiwanda

- Amekosa kipato cha kila siku

- Alikuwa anapanga ila kwa kukosa mshahara inabidi arudi nyumbani kuanza upya

- Alikuwa anakula kwa mama ntilie mchana akiwa kazini, ina maana yule mama amekosa wateja kwahiyo na yeye inabidi afunge mgahawa wake.

- Alikuwa anapanda daladala kila siku, inamaana mwenye biashara ya daladala amekosa mteja.

- Alikuwa anapanda pikipiki akitoka kazini, ina maana mwenye bodaboda na yeye amekosa mteja.

- Alikuwa analipa gym kwa mwezi sema ameona awe anaingia mara 3 tu kwa week, kwahiyo mwenye gym na yeye kapoteza mteja anayelipa kwa mwezi nk



Mfano 2:

Aliyekosa kodi ya jengo kutokana na kufungwa kwa kiwanda

- Kakosa uhakika wa kodi ya kila mwezi kutoka kwa mwenye kiwanda.

- Alikuwa na frame nyengine pembeni ambazo zilijaa kutokana na uwepo wa kiwanda, kufungwa kwa kiwanda wenye frame na wao wameachia frame kwasababu hakuna tena mzunguko wa pesa.

- Ukosefu wa kiwanda katika lle eneo basi thamani ya frame nayo imeshuka kwa kiasi kikubwa, kwahiyo inabidi apangishe kwa kodi ndogo.



Mfano 3:

Serikali

- Serikali imekosa kodi ya uzalishaji iliyokuwa inapatikana kwenye kile kiwanda.

- Serikali imekosa P.A.Y.E kutoka kwa wafanyakazi wa kile kiwanda.

- Serikali imekosa pesa zake za HESLB kutoka kwa waliokuwa wameajiriwa na kiwanda hicho.

- Serikali imekosa wanachama wa NHIF waliokuwa wameajiriwa katika kiwanda hicho.

-Serikali imekosa pension walizokuwa wanawekewa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Kwahiyo kufeli kwa mtu mmoja huenda kukasababisha kufeli kwa dunia nzima taratibu.

Ila good news ni kwamba kila kitu hupita ni swala la muda, mambo yatabadilika na kuwa mazuri tena.

#depression #trough #uchumi #economics #multipliereffect
 
Back
Top Bottom