Ugumu wa maisha ya mtaani ukilinganisha na maisha ya Chuo

Chatterman

Senior Member
Joined
May 25, 2024
Posts
185
Reaction score
378
Kama ikitokea siku mtu akakuhitaji umuweke bayana kati ya Life la Chuo na la Kitaa ni lipi lina songombingo nyingi basi vuta pumzi kisha mwambieee 'hakuna Embe litakaloweza kuota kwenye Mnanasi na hakuna Nanasi litakaloota kwenye tawi la Muembe'

Hali kadhalika ukiwachukua watu wawili. Mmoja awe mtu wa kitaa maisha yake yote na wapili awe Mwanachuo ambaye bado yupo masomoni basi hawa watu vilio vyao ukivisikia kila mmoja utaona anavyokipamba cha kwake.

Hata kama mkiandaa Midahalo MILIONI Mia Saba Sabini na Saba laki Saba elfu Sabini na Saba mia Saba Sabini na Saba kwa siku 7 mara 7 hadi siku ya saba saa 7. Basi Haitajalisha mshindi atakuwa nani na atashinda mara ngapi, bali la muhimu ni pande zote kufika katika HADHINA YA MAFANIKIO.

Hivyo sikushauri kudharau watu wa mtaani na pia sikushauri kudharau waliopo chuoni kwani zote ni nyakati za utafutaji.

Na ukiamua kukaidi basi hongera kwa kuutumia vizuri uhuru wako. Huenda utafaidi utakuwa mkaidi wa kwanza kufaidi siku ya Idi (EID)

Hiyo isikuchekeshe bali ikufikirishe.
Walau ukitaka majibu ya kuridhisha mtafute mtu aliyefanikiwa kuishi nyakati zote mbili na kwa hali duni. Yaani mtafute aliyekuwa chuo na sasa yupo kitaa kisha akujuze namna alivyopitia nyakati zote mbili.

MSINGI WA HILI NI NINI.
Kulinganisha maisha kati ya Kitaa na maisha ya Chuo Kikuu ni kama kulinganisha maajabu mawili tofauti. Maisha ya Kitaa yana upekee wake, kama vile uhuru zaidi na uwezo wa kujitegemea, wakati maisha ya Chuo Kikuu yanakuja na majukumu ya masomo, fursa ya kujifunza kutoka kwa wenzako, na uzoefu wa kujenga mtandao wa kijamii na kitaaluma. Kwa wengine, maisha ya kitaa yanaweza kuwa na changamoto za kifedha au usalama, wakati maisha ya chuo kikuu yanaweza kuwa na shinikizo za kitaaluma na kijamii. Kwa ujumla, kila mtu anaweza kupata uzoefu tofauti kulingana na malengo yao na mazingira yao ya kibinafsi.

LA KUZINGATIA.
Ikumbukwe kuwa Maisha ya kitaa ni maisha yasiyokwepeka haijalishi utasoma miaka miangapi. Sio wote watakao bahatika kusoma ila wote tutakutana kitaa.

Kujua utaingiaje kitaa ni jambo la msingi kuliko yote, alkadhalika kujenga uhusiano mzuri na wana wa kitaa ni kuandaa watu wa kukupokea na mazingira mazuri ya Mipango yako ukiwa kitaani. Aidha biashara au Ajira.

Ni dhahiri hatuwezi yalinganisha maisha ya Chuo na ya Kitaa walakini Hustle za Chuo na Harakati za kitaa zote ni katika kusaka shilingi ya kutoboa kimaisha. Hivyo hata kama hatufanani kihivyo basi jua wote tunalenga shabaha moja.

HITIMISHO:
Ugumu wa chuo aujuaye Msomi.
Ugumu wa kitaa aujuaye Msaka shilingi.

"SIWAFUNDISHI bali NAWAKUMBUSHA".
Kwa maana imeandikwa; sina akili kuwazidi 🫡
 
Nnnyaaa! Uekeweki!
 
Ni kama unawatisha hivi ila ndo ukweli wanaopaswa kuujua
Si tushapitia kote usiombe kabisa kufanya kazi chini ya tamisemi mfano mzuri hawa walim na watu wa afya na hawa sijui maafsa kilimo mifugo yaan acha kabisa usipojiongeza mtaani wanaishi kwa tabu sn yaan mtu yupo chaka kachakaa bora hata bodaboda ana life lenye kueleweka
 
Huu ni ukweli mtupu tena mchungu sana.
 
Kwa kifupi
• Uliye mtaani usimdharau anaeenda kusoma kwa sababu unajiona tayari kuna mafanikio fulani mbeleni.

Na pia uliye chuoni usimdharau uliyemuacha mtaani kwamba yeye ni failure.

Mwisho wa siku wote tunategemeana,asiyesoma akishikwa malaria atenda kumuona doctor au akiwa na errors na TRA ataenda kumuona muhasibu waliomuacha mtaani wakaenda chuoni same kwa aliyeenda chuo akirudi mtaani atategemea huyu aliyemuacha mtaani amuhudumie kwa kile alikifata chuo.
 
Nikupata uzuri sana
 
Si tushapitia kote usiombe kabisa kufanya kazi chini ya tamisemi mfano mzuri hawa walim na watu wa afya na hawa sijui maafsa kilimo mifugo yaan acha kabisa usipojiongeza mtaani wanaishi kwa tabu sn yaan mtu yupo chaka kachakaa bora hata bodaboda ana life lenye kueleweka
Mwalimu kaitoa nchi mikononi mwa wakoloni leo anapangiwa mshahara na mwanasiasa.
 
Acha kufananishaa life la mtaani na vitu vya ajabu

Life La mtaani.....degree haifanyi kazi, usister duh au handsome wako ndo kabisa watu hawajari, loose hope hakuna heshima kwa wakubwa nawadogo,...n.k
 
🤣🤣🤣
Ikitokea mwalimu anafundisha unapaswa kukaa dawati la Mbele
Nanukuu nilichotype: 👇
"Kulinganisha maisha kati ya Kitaa na maisha ya Chuo Kikuu ni kama kulinganisha maajabu mawili tofauti".
Sikulaumu utakuwa ulivua miwani.
 
Aaah sawa mkuuu nimekuelewaaa mtaani kama shetani aliyesahau chupi mbinguni
 
Back
Top Bottom