Ugunduzi mpya kuhusu Malaria

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Kulingana na uchunguzi vimelea vinavyosababisha Malaria huweza kuishi mwilini kwa uboho (bone marrow) na kuepuka kinga za mwili na hivyo basi kusababisha maradhi.


Uchunguzi huu umedhihirishwa na bwana Marti ambaye alizungumza na BBC.

Swala la vimelea hivyo kujificha kwa uboho si jambo geni, lakini kundi la wanasayansi wakiongozwa na Profesa Matthias Marti katika idara ya Afya ya umma kule Harvard, Boston, walifichua hasa ambako vimelea hivyo hujificha na kutoa maonyesho.


Uzinduzi huu una umuhimu mkubwa kwa misingi kuwa umeleta ujuzi unaohitajika sana na huweza kupelekea kuundwa kwa dawa na kinga mpya za kukabiliana na vimelea hivyo ili kuzuia maambukizi.


Kwa mujibu wa wanasayansi huko Harvard, uchunguzi huu uliochapishwa na jarida la kisayansi la Science Translational Medicine, umeongeza ujuzi wa kibayologia utakaotumika kuchunguza ugonjwa wa Malaria hata zaidi.


Vimelea vinavyosababisha Malaria huambukizwa hasa kupitia Mbu, na husababisha vifo zaidi ya nusu kila mwaka ulimwenguni.


Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Shirika la afya duniani, zinapendekeza kuwa Malaria ilisababisha vifo laki sita mwaka wa 2012, na takriban asilimia tisini ya vifo hivyo vilitokea Afrika. Chanzo.BBC
 
So ndo mana naumwa mgongo nini na viungo vyote vya mwili,aisee mkuu naomba msaada wa dawa ya malaria inanisumbua sana.Nimetumia Zandu Za kihindi na Madawa mengine bila mafanikio
Mgongo unauma sana nyakati Za Usiku hata silali aisee
Cc MziziMkavu
 
So ndo mana naumwa mgongo nini na viungo vyote vya mwili,aisee mkuu naomba msaada wa dawa ya malaria inanisumbua sana.Nimetumia Zandu Za kihindi na Madawa mengine bila mafanikio
Mgongo unauma sana nyakati Za Usiku hata silali aisee
Cc MziziMkavu

TIBA YA MALARIA


Ugonjwa wa malaria umekuwa na tiba za asili nyingi ambazo baadhi tumeshaziandika na zimewasaidia wengi, leo tunawaletea tiba nyingine inayomaliza kabisa maradhi hayo.

Bamia
Chukua mbegu za bamia uzikaange, uzisage mpaka ziwe unga.
Chemsha nusu kikombe cha unga huo katika glasi 2 za maji kisha chuja.

Dozi:
Wakubwa kikombe 1 x 3 kwa siku kila baada ya mlo.
Miaka (7-12 ) anywe nusu kikombe x 3 kwa siku kila baada ya mlo. Huruhusiwi kuchemsha na kuweka bali fanya hivyo kila unapotaka kunywa.
Miaka (2-6) robo kikombe x 3 kwa siku.
Kwa watoto wachanga kijiko kikubwa 1 x 3, mpatie baada ya kunyonya au kunywa maziwa na kushiba.

Papai

Chukua mbegu za papai zikaushe kivulini, baada ya hapo zisage ziwe unga laini.

Dozi:
Weka kijiko kimoja cha chai kwenye uji, kama huwezi kutumia uji unaweza kuweka kwenye chai lakini muhimu sana kwenye uji.
Kwa siku tumia mara tatu.
Kwa mtoto miaka 5-10 unaweza kumgawia nusu ya mtu mzima.
Kwa mtoto wa miaka 3-5 unaweza kumgawia ¼ wote x 3 kutwa.

Alizeti
Chemsha kilo moja ya majani ya alizeti katika lita 2½ za maji kwa dakika 15. Dozi:
Kunywa nusu glasi x 3 kwa siku, tumia tiba hii kwa muda wa siku 5.
Miaka (7-12) ¼ glasi x 3 kwa siku. Miaka (2-6) kijiko 1 x 3 kwa siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…