Ugunduzi, uzalishaji wa gesi unavyoendelea kuleta manufaa

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
552



TANZANIA ni nchi yenye rasilimali nyingi na zenye tija kwa taifa kama zitavunwa kwa njia endelevu kupitia mikataba yenye tija baina ya Tanzania na kampuni za kimataifa zinazomiliki teknolojia na mitaji. Gesi asilia, kama ilivyo kwa madini, ni rasilimali nyingine muhimu inayopatikana kwa wingi Tanzania lakini ambayo uvunaji wake unahitaji mtaji mkubwa na teknolojia ya kisasa.

Ni katika muktadha huo, Tanzania imeweka sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za kusimamia uzalishaji wa gesi asilia nchini. Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ndilo lenye dhima ya utafutaji, maendeleo, uzalishaji na usambazaji wa mafuta, gesi sambamba na huduma zinazohusiana na bidhaa zitokanazo na gesi asilia.

Huduma hizo ni kama vile uendelezaji kwa kuweka mazingira mazuri ya kibiashara, kulinda upatikanaji wa bidhaa za mafuta na gesi, wakati huo huo likiandaa viwango vyenye ubora ili kulinda watu, mali na mazingira. Kwa kifupi, Sheria mpya ya Mafuta ya mwaka 2015 inaipa majukumu mapya TPDC ambalo sasa litajikita kwenye biashara zaidi kama Kampuni la Umma ka Mafuta kuliko kutoa huduma.

Kupitia maswali ya mwandishi wa makala haya yaliyoelekezwa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji wa TPDC, Kapuulya Musomba, mpaka sasa kuna kampuni nane za kimataifa zilizopewa leseni kwa ajili ya shughuli mbalimbali zinazohusiana na sekta ya mafuta na gesi nchini.


Taarifa hiyo ya TPDC kwa gazeti hili inasema kati ya kampuni hizo nane, tatu zina leseni ya uzalishaji au uendelezaji wa mafuta na gesi ambazo ni Pan Africa, Maurel and Prom na Ndovu Resources. Msomba anasema kampuni tano zilizobaki zina leseni za utati ambazo ni pamoja na Ndovu Resources, Swala Energy, Equinor, Shell, Heritage na Dodsal. Taarifa inafafanua kwamba kampuni hizi pia zina washirika wengine kutoka nchi mbalimbali ambao wanafanya kazi kwa pamoja kwenye leseni zao zilizotolewa na Serikali.

Hadi sasa kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa nchini ni futi za ujazo (TFC) trilioni 57.54. Hii inajumuisha gesi yenye futi za ujazo trilioni 10.406 iliyogunduliwa nchi kavu huku kwenye bahari kuu kuwa na futi za ujazo trilioni 47.13 zilizogunduliwa. Uzalishaji wa gesi baharini Akijibu swali ni lini uzalishaji utaanza katika vitalu vilivyopo baharani, Kaimu Mkurugenzi Musomba, anasema kwamba kutokana na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kitalu namba moja hadi nne, Serikali na Kampuni ya Shell, Equinor, ExxonMobil, Ophir na Pavillion zilikubaliana kuendeleza gesi iliyogunduliwa kwa njia ya LNG (Liquied Natural Gas). Anasema kwamba kwa kawaida utekelezaji wa miradi ya LNG duniani huchukua miaka minane hadi 10 kuanza (ikiwemo baada ya mazungumzo na serikali kukamilika).

Kwa mujibu wa TPDC chochote ambacho kitagunduliwa, iwe ni mafuta au gesi, mgawanyo wa mapato utakuwa ni kati ya TPDC (NOC) na huyo mwekezaji. Na kwamba TPDC anasimama hapo kuwasilisha umma na hivyo kila mwekezaji anayekuja Tanzania, serikali inapata mgawo wake kupitia TPDC.

Anasema ujenzi pekee wa miundombinu huchukua miaka mitano, ikiwa ni pamoja na matayarisho yanayohusisha stadi na tafiti za awali na za kina za kihandisi ambazo huchukua mwaka mmoja na nusu hadi miaka miwili kukamilika. Kwa mujibu wa TPDC, utekelezaji wa mradi wa LNG kwa sasa uko katika hatua ya majadiliano kati ya wawekezaji na serikali.

“Kama majadiliano yataenda kama ilivyopangwa, ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwaka 2021/22,” anasema Musomba. Ili kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa, na nchi haipati hasara kwa sababu ya mikataba mibovu, Musomba anasema serikali imeunda timu ya majadiliano (GNT) yenye wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.

Sambamba na kuwepo kwa GNT Musomba amasema Serikali iko katika mchakato wa kumpata Mshauri Mwelekezi ambaye atasaidia katika majadiliano hayo ili kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa na nchi haipati hasara. Taarifa za TPDC zinaonesha kwamba mpaka sasa kuna faida nyingi zinazotokana na ugunduzi wa gesi nchini mwetu lakini pia unaweza kuiona kwenye mchango inayotoa katika pato la Taifa.

Katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2015 ambapo mradi wa bomba la gesi ulianza kufanya kazi, taarifa inasema mbali na kuongeza uhakika wa umeme nchini, kiasi cha shilingi bilioni 69 ambazo zinatokana na mrabaha na gawio la faida ya uzalishaji wa gesi asilia zimepelekwa serikalini.

Kodi iliyolipwa katika kipindi hicho ni kiasi cha Sh bilioni 118 huku Dola za Marekani bilioni 3.2 zikiokolewa kutokana na kuchochea matumizi ya gesi asilia badala ya mafuta mazito viwandani na katika kuzalisha umeme. “Si hivyo tu, ugunduzi wa gesi asilia hapa nchini umeifanya nchi yetu kuvutia zaidi uwekezaji kutoka nje ya nchi (Foreign Direct Investment) ambapo, kama tulivyokwishaeleza kuna makampuni takribani nane ya kimataifa ambayo yamewekeza hapa nchini kwa sasa katika utati na uendelezaji wa mafuta na gesi.

Ugunduzi wa mafuta bado Kwa mujibu wa Musomba hadi sasa, Tanzania bado haijagundua mafuta. Hata hivyo, anasema kuna viashiria vingi ambavyo vinaonesha uwepo wa mafuta katika maeneo mbali mbali ya nchi. Anataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na Wingayongo, Tongoni, Tambarani, Ziwa Tanganyika na Pemba ambapo michirizi ya mafuta inayojulikana kama ‘oil seep’ kwa kitaalamu imeonekana
 
Acha uongo, makampuni yote ya gas yalishaondoka Mtwara. Wamebaki Morel Prom peke yao ambao wanauza gesi TANESCO Mtwara.
Songas Pan African Energies wao wako Songosongo.
Kwenye sekta ya gesi ni kama tunazalisha 0.000005% ya uwezo tulionao kuzalisha.
Gas sio kipaumbele cha serikali ya Magufuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…