Uhaba wa ajira Serikalini

Uhaba wa ajira Serikalini

Cesar Saint

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2016
Posts
423
Reaction score
726
Umewahi kufikiri inawezekanaje nchi kubwa kama Tanzania kuwe na upungufu wa ajira tena sio tu kwenye sekta binafsi bali hali ni mbaya zaidi Serikalini .

Kumekuwa na mazoea kuifanya hali hii kuwa ya kawaida kiasi kwamba kwa vijana wanaoingia vyuoni kuambiwa wanatakiwa kusoma vitu watakavyoweza kuajiriwa au kujiajiri.

Miongoni mwa jambo kubwa linalochelewesha pengine hata kufubaza maendeleo ya nchi nyingi za Kiafrika ikiwemo Tanzania ni uwepo wa uhaba mkubwa wa watendaji (wafanyakazi) katika sekta na nyanja mbalimbali za kijamii.

Turudi nyuma kidogo na kuangalia mzizi wa tatizo! Wakati nchi yetu inapata uhuru kulikuwa na idadi ndogo ya wasomi na hata ambao walikuwepo walisomea elimu zilisotumiwa kusukuma shughuli za kikoloni na hivyo kuilazimu Serikali ya wazawa kuanza kutumia ile nguvu kazi ya wageni iliyokuwepo katika maeneo mbalimbali.

Jitihada zikafanyika ikiwa pamoja na kusomesha vijana wazawa na kuwajenga katika misingi mizuri ya kuhudumia na kujitoa katika utumishi wa Uma.Kwa sehemu yao kizazi hiki kilifanya na huku kikiweka misingi ya kuendelea kuzalisha wasomi wa kulitumikia taifa katika nyanja mbalimbali.

Mifumo hii ya uzalishaji wasomi pamoja na mapungufu yake bado imeendelea kuzalisha wasomi katika taifa letu kila uchwao tena wakati huu kasi ya kuzalisha wasomi si sawa na ile ya hapo awali wakati nchi ilipojipatia uhuru.

Chimbuko la Tatizo

Tatizo la ajira lilianza pale kasi ya uzalishaji wasomi ilipozidi kasi ya upanuzi wa shughuli za kimaendeleo na kimkakati katika kuinua taifa.

Si kwamba Serikali au mifumo ya kiserikali au nyanja mbalimbali za shughuli za Serikali hazihitaji wafanyakazi (wasomi) bali uwezo wa Serikali yetu kumudu kuwahudumia vijana hawa waliandaliwa kujenga taifa ni mdogo na huu ndio ukweli mchungu .

Leo hii kumekuwa na usimamizi na utendaji wa shughuli za kiserikali kutokana na upungufu wa rasilimali watu katika maeneo husika na kuilazimu nguvukazi iliyopo kwenye eneo husika kufanya majukumu ambayo haikuandaliwa nayo.

Unaenda sehemu unakutana na daktari yeye ndio mhasibu,yeye ndio afisa manunuzi na yeye ndio afisa tehama.Si ajabu kukuta shule ambayo mhasibu ndio afisa manunuzi huku mwalimu mmoja aliyechangamka akawa ndio mwongoza mfumo (Tehama) wa shule husika.Au unakutana afisa mipango anayefanya majukumu ya afisa mazingira.

Unajua kuwa miongoni mwa sababu kubwa ya Serikali kufanya vibaya kwenye miradi yake ni ukosefu wa watendaji?

Serikali inaenda kuwekeza mradi wa billions kwenye eneo lenye uhaba mkubwa wa watu wa kusimamia uendeshwaji wa shughuli za kila siku .

Na mbaya zaidi unakutana na ofisi nyingi ambazo watu hufanya majukumu ya watu wengine kutokana na uhaba wa wafanyakazi au mtu husika wa taaluma au eneo hilo.

Nini kifanyike
Serikali ina wajibu wa kutengeneza mazingira na fursa zitakazoweza kuwajengea uwezo wasomi (nguvu kazi) hii inayopotea ifanye elimu zao kuwa biashara na waweze kujiajiri kutoa huduma ya kile walichosomea kwenye jamii .

Kwa kuanzia inaweza kutoa grants kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu ili waweze kuanzisha vitega uchumi mbalimbali hii itawafaa zaidi hasa kwa zile course zisizopewa kipaumbele.

Vijana waandike proposal ambazo zitapitiwa na tume ya vyuo vikuu na kushindanishwa ambapo kundi la washindi wenye proposal husika watawezeshwa kifedha au vitendea kazi kulingana na proposal yao kwa mkopo usio na masharti makali. Huu ni uwekezaji wa moja kwa moja wa Serikali kwa watu wake .

Pili ,Vyuo vitoe kipaumbele kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo husika kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya vitega uchumi vilivyopo chuoni.

Ni aibu chuo kikongwe UDSM kukosa hata sehemu ndogo ambayo wanafunzi/graduates wamewezeshwa kufanya shughuli za kiuchumia katika economic center kama ile ya mlimani city mall.

Hivi kweli tumeshindwa hata kuwa na festival mara moja kwa mwezi ambapo wanafunzi walianzisha biashara zao wangeweza kufanya maonyesho katika eneo lile?

Au kutenga eneo ndani ya mall ambapo mwanafunzi/graduate atawekeza kwa muda wa mwaka kisha kupisha mwengine akikaa na kutumia eneo hilo kwa kodi nafuu atakayoweza kumudu.

Tatu ,Serikali inapaswa kuajiri
Ili tuweze kufikia mahali ambapo sisi kama taifa tunataka kufika ni lazima serikali itengeneze mazingira ya kuajiri watu wake.
Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe hivyo nguvu kazi iliyopo inapaswa kutumika.

Serikali inapaswa kuajiri watu katika nyanja zote ili tupate mabadiliko ya kiundendaji kwani kutakuwa na ongezeko la utendaji.Wakiwepo walimu wanne wa biology katika shule flani matokeo yao ufaulu na uelewa wa wanafunzi hauwezi kuwa sawa na wale wenye mwalimu mmoja kidato cha kwanza mpaka cha nne.

Hatuwezi kuwa nchi inayolala yote usiku na tukategemea kupata maendeleo ya uhakika.Yaani ukipita city center usiku hakuna shughuli inayofanyika! Shirika kama Tanesco unakuta kanda nzima kuna gari moja ya emergency kweli tuko serious na maendeleo? Kinachozuia kusiwe na shift za usiku ni uhaba wa watu.

Hitimisho
Ajira ni maisha ya kila siku .Vijana na wadau wote wa maendeleo tunajukumu la kuzifanya elimu zetu kuwa AJIRA .

Au kwa lugha nyepesi mfumo wa elimu yetu unapaswa kuwajengea wasomi uwezo wa kufanya au kugeuza elimu zao kuwa biashara.
 
Maendeleo ya wananchi ni lazima, kuwe na uzalishaji wa ndani na kuuza soko la nje.

Sasa bongo hapa tunazalisha nini? Sisi ni wateja wazuri wa kununua bidhaa za watu tu. Stupid 😩
 
Maendeleo ya wananchi ni lazima, kuwe na uzalishaji wa ndani na kuuza soko la nje.

Sasa bongo hapa tunazalisha nini? Sisi ni wateja wazuri wa kununua bidhaa za watu tu. Stupid [emoji30]

Kuna kipindi ilisemekana ni mikataba ya “kimaendeleo” tunayoingia inatulazimu kuwa wateja wa wadai wetu .
Lakini kwa nguvukazi tulionayo kama taifa hata hii Tanzania ya viwanda tunayoimba inawezekana.
Tatizo letu kubwa watu wenye dhamana ya kufanya maamuzi wanakula viyoyozi tu .
 
Kuna kipindi ilisemekana ni mikataba ya “kimaendeleo” tunayoingia inatulazimu kuwa wateja wa wadai wetu .
Lakini kwa nguvukazi tulionayo kama taifa hata hii Tanzania ya viwanda tunayoimba inawezekana.
Tatizo letu kubwa watu wenye dhamana ya kufanya maamuzi wanakula viyoyozi tu .
Bongo tutasota sana na hii CCM yetu ambayo kila Rais anae ingia anakuja na mambo yake anayojisikia yeye kufanya.
Wananchi tunapambana sanaa, kama biashara ndogo ndogo tu kwa sana.
 
Binafsi ni muumini wa udogo wa serikali na ukubwa wa sekta binafsi. Serikali haiwezi kuajiri kila mtu mwenye sifa ya kuajiriwa. Si kazi yake. Kazi ya serikali ni kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji na utendaji katika sekta binafsi, na yenyewe serikali kukaa kando: eyes-on, hands-off.
 
Back
Top Bottom