Uhaba wa mafuta wakwamisha kesi ya mauaji ya Mwangosi

Uhaba wa mafuta wakwamisha kesi ya mauaji ya Mwangosi

tembeleh2

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2010
Posts
765
Reaction score
166
UHABA wa mafuta umeendelea kuleta usumbufu mikoani na hivyo kusababisha kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, kushindwa kusikilizwa jana kutokana na mtuhumiwa kushindwa kufikishwa mahakamani.Mtuhumiwa huyo, ambaye ni askari polisi, Pasificus Cleophace Simon (23), anayedaiwa kumuua Mwangosi, alishindwa kufika mahakamani kutokana na gari la kubebea mahabusu kutokuwa na mafuta.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya, Dyness Lyimo, alisema Pasificus na watuhumiwa wengine waliopo mahabusu hawakufikishwa mahakamani kwa sababu ya gari linalotumika kuwapeleka halikuwa na mafuta.


"Tatizo kubwa lililopo sasa hivi ni uhaba wa mafuta kwa sababu hata mimi mwenyewe gari langu halina mafuta…sisi tunategemea mafuta kutoka boharini na kwa bahati mbaya hayapo," alisema. Hata hivyo, Lyimo alisema kuwa kulikuwa na uwezekano wa kumpeleka Pasificus kwa miguu kutokana na gereza hilo kuwa jirani na mahakama, lakini hawakufanya hivyo ili kuzuia kuteka hisia za watu na kuepusha fujo."Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa watuhumiwa kuletwa mahakamani kwa miguu, lakini haikuwezekana kwa sababu askari wasingeweza kumchukua mtuhumiwa mmoja na kuwaacha wengine ambao walipaswa kusomewa mashtaka yao hapo leo," alisema.

Haya jamani sijui nchi hii inaelekea wapi!!!!

Source: Tanzania daima
 
Back
Top Bottom