BY DR. Engutan-K
Kisukari ni ugojwa wa chachu ( Hormonal desease),
Kisukari ni hali ya kuwepo sukari nyingi kwenye damu au kwenye mishipa ya damu wakati inatakiwa iwe kwenye nyama yaani tissue au cells kwani kule kwenye cells sukari hiyo huunguzwa ili baadae itoe nguvu (enegy) ambayo hukusaidia wewe kufanya kazi mfano kukimbia, kutembea, kufikiri, kufua, kujamiiana n.k
Uwepo wa sukari nyingi kwenye mishipa ya damu nitafananisha na pale Kongwa ranch ukipita huwezi kuzionan ng`ombe kwa urais kwani zinakuwa zimetawanyika mbugani zikichunga lakini siku ukipita ukakuta ng`ombe zote zimelala barabarani yaani zimelala kwenye barabara ya lami toka Kibaigwa hadi Mbande tafisiri yake siyo ng`mbe za ranch ya Kongwa zimeongezeka ni zile zile bali zimekaa mahali ambapo si sahihi ziwepo kwa wakati ule bali zinatakiwa ziwe mbugani zinachunga.Na kisukari hivyo hivyo siyo kwamba inakuwa ni nyingi ni ile ile bali kwa wakati ule huwa haitakiwi iwe kwenye mishipa ya damu bali ipite yu iende kwenye nyama ambapo ndo kiwandani ili isagwe itoe nguvu.
Kutokana na mfano huo juu ni jukumu la wachungaji kuzifukuza zile ng`ombe zilizolala barabarani zitoke pale zilipo ziende mbugani zikachunge, kwa kisukari wachungaji hao ni chachu fulani (hormone) inaitwa INSULIN, Insulin hii hutoka kwenye tezi fulani inaitwa KONGOSHO kiswahili ambayo ni vifutafuta fulani chini ya tumbo ndani au jina lingine la kitaalamu huitwa Pancries. Kazi ya chachu hii INSULIN ni kuisukuma sukari toka kwenye mishipa ya damu iende kwenye nyama ikasagwe itoe nguvu.
Tukirudi kwenye mfano wa juu ngo`mbe kulala barabarani kunaweza kuwa kumetokana na wachungaji kuwa ni wachache na kundi ni kubwa, wachungaji hao wengine wanaweza kuwa wamakufa au wameacha kazi au wamestaafu kwa hiyo ni jukumu la mwajiri kuongeza wachungaji wengine wapya.
Hivyo hivyo hata kwenye kisukari, sukari nyingi inaweza kuwa kwenye mishipa ya damu kutokana na upungufu wa hormone Insulin unaotokana na mahitaji yamekuwa makubwa yaani mhusika anaingiza corbhaydrate kwa wingi ambayo hubadirika kuwa sukari, watu wenye hali nzuri kiuchumi hula corbohadrate kwa wingi kuliko mahitaji na uwezo wa insulin zao inakuwa ni mdago kuisafirisha yote itoke kwenye damu iende kwenye nyama kwa hiyo huhitaji kupewa Insulin ya ziada.
Nimechoka kueleza zaidi mleta mada asome aelewe kwamba kisukari kinatokana na kuingiza corbohydrate kwa wingi kutokana na uwezo wao kiuchumi yaani mfano mtu anakula pombe nyama mwaka mzima kilo zinaongezeka hadi insulin inashindwa kumudu majukumu yake.
Cha kuepuka ili sukari isiwe nyingi siyo sukari kama mleta mada alivyozani bali ni kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga yani pombe, nyama,chapati, wali, ugali , mchele na maziwa kifupi ni vitu vyote vitamu vutamu ukivila , nini kitamu kama nyama, kisukari inabidi uaachane na nyana au upunguze sana kuila.
Nimchekeshe mleta mada kama kuepuka kisukari ni kuacha kutumia vitu vyenye sukari kama soda AU chai na vingine kila mtu angeweza ila kuepuka kisukari ni lazima uachane na vitu vingi hivyo nilivyokutajia sukari yenyewe ikiwa ni mwisho kabisa.
UKITAKA KUJUA ZAIDI NI PM.