holoholo
JF-Expert Member
- May 10, 2023
- 1,859
- 2,986
Uhaba wa walimu imekuwa ni janga la kitaifa kwa shule za msingi za maeneo ya vijijini, shule yenye wanafunzi karibia 600 ina walimu wanne, walimu wanahama bila mpangilio, lakini hawaletwi wapya, imefikia wananchi tunachanga fedha kwa ajiri ya kuajiri walimu wa muda kuokoa watoto wetu.
Nimetoka kwenye kikao cha wazazi muda huu kujadili namna gani tunafanya ili wawepo walimu wa muda ili kuwasaidia hawa wanne waliobaki.
Hali ni mbaya mashuleni, watoto wetu tumewaachia waende shule lakini hawaambulii kitu badala yake wanaenda kucheza tu walimu hamna.
Tafadhari Serikali liangalieni kwa jicho la tatu.