Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Kuna baadhi ya michakato (processes) na itifaki (protocols) ambazo tulirithi toka kwa wakoloni na awamu zilizopita ilikuwa muhimu wakati ule sababu office automation haikuwepo. Kwa sasa hali ni tofauti baada ya maendeleo makubwa ya teknolojia ya mawasiliano.
Kuwadai watu wanao omba kazi au mikopo elimu ya juu waende kuhakiki vyeti kwa mwanasheria au RITA ni matumizi mabaya ya rasilimali muda na watu.
Sasa kuna mifuo ya tehama karibu kila idara ya serikali
.
Umeweka shariti maombi husika yaambatanishwe na nakala (copy) ya cheti halisi, umemuambia ajaze namba zake za cheti cha kuzaliwa au cha shule au chuo. Inakuaje tena umwambie aende akahakiki kisha afanye nakala ya kielektroniki hicho cheti kilicho thibitishwa awatumie hamjui kwamba unaweza kukifanyia ujanja hiyo nakala dijitali ukabadili jina au picha ya mtu?
Mtu akiitwa kwenye usahili au akienda kujisajiri kwenye vyuo ambako atalipiwa mkopo si wanahakiki vyeti halisi (original) kujiridhisha aliyetuma taarifa siyo tofauti na aliyekuja chuo au vyeti alivyotuma ni vyake na halisi?
Kwanini nyie msichukue zile namba zake za cheti na picha mkalinganisha na taarifa zilizopo kwenye kanzidata (database) ya taasisi iliyotoa hicho cheti?
Mnawaongezea kazi nyingi zisizo na ulazima hizo tasisi kama RITA kisha wanaanza kuzidiwa na majukumu na kujikuta wanafanya vibaya baadhi ya majukumu yao.
Kwanini mtu akishatuma taarifa zake mifumo isihakiki? Mambo haya ndiyo yanalalamikiwa sana na wawekezaji yanaongeza urasimu na kuchelewesha mambo.
Kama mnataka kupunguza usumbufu wa watu wanao ghushi (forge) vyeti bandia (fake) muweke utaratibu mzuri wa kuwalipisha fidia waliowasumbua na kutekeleza adhabu ya kifungo ili watu waogope. Pia mtajipatia kipato cha ziada kwa hizo faini.
Tuache duplication ya activities flani kama inawezekana kuepuka kufanya hivyo na kuokoa muda. Kama inawezekana kumaliza jambo mtandaoni(online) basi limalizwe haraka tuache mizunguko na kutengeneza vichaka vya watu kutoa au kuombwa rushwa za elfu kumi kwenye uhakiki.
Mbona simu banking au fedha za mitandaoni (internet banking) tunapata huduma za mamilioni mengi pengine kuliko ya mkopo wa HESLEB baada ya mifumo kuhakiki taarifa alizotuma mteja kwenda bank kwa mfumo huo wa kielektroniki na hakuna ulazima wa kwenda kuhakiki taasisi yoyote?
NOTE: Haya ni maoni binafsi tu, hivyo nakaribisha kukosolewa au kusahihishwa na kuoneshwa ulazima wa kufanya inavyofanyika.