Uhakiki wa Kazi

Red Scorpion

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,736
Reaction score
4,252
TUKIACHA UHAKIKI VYETI, HUU HAPA NI UHAKIKI KAZI.

Hapo kale kuna kijana alifika kwenye kibanda cha simu, baada ya kulipia huduma alikwenda kwenye chumba maalum na kupiga simu. Mmiliki wa kibanda cha simu, alikuwa akisikiliza mazungumzo yake.

Kijana: "Samahani Madam, ninaitwa Daudi. mimi ni dereva mwenye uzoefu mkubwa. Tafadhali ninaweza kupata kazi ya kukuendesha?"

Madam : (upande wa pili wa simu) "Oh, tayari ninaye dereva wangu."

Kijana: "Madam, tafadhali nisaidie kazi, nitakuendesha kwa nusu ya mshahara unaomlipa dereva wako wa sasa."

Madam: "Hapana, ninaridhishwa na utendaji wa dereva wangu bila kujali ninachomlipa."

Kijana: (Kwa heshima na utii) "Je, madam ninaweza kupata japo ufundi tu wa gari lako, miye pia ni fundi mzuri sana."

Madame: "Hapana, dereva wangu ni fundi mahiri pia."

Kijana alikata simu na kuurejesha mkonga mahala pake. Akiwa anataka kuondoka, mmiliki wa kibanda cha simu alimwita yule kijana.

Mmiliki: "Kijana, nimependa ari yako katika kutafuta kazi. Nimesikitika umeikosa hiyo kazi. Lakini, sasa nataka nikuajiri."

Kijana: "Ahsante mkuu. Lakini sihitaji kazi yako."

Mmiliki: (Kwa mshangao) "Lakini nimekusikia ukibembeleza upate kazi japo ya ufundi tu! Mi nataka kukupa kazi ya udereva wa gari yangu na ufundi wake."

Kijana: (Huku ametabasamu) "Hapana mkuu, sikuwa nikitaka kazi. Nilikuwa nikihakiki ufanisi wangu katika kazi. Mimi ndiye dereva wa huyo madam niliyekuwa nikiongea naye simuni. Nilitaka kuona kwa namna navyomfanyia kazi anaridhika, au siku akitokea mtu mwingine, atanifukuza?"

FUNZO: Ukifanya kazi kwa bidii, uaminifu na utii. Kwa yakini utapata mradi wako huku ukiwa na uhakika wa nafasi yako, hata kama atatokea mtu wa kutaka kukufitini ili kukuondosha kazini. Unaweza kuhakiki kazi yako kama ni kweli unastahiki kuendelea nayo.
 
Aseee we jamaa Unaakili sana. Hongera!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…