BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Kamishna Msaidizi wa Polisi Michael Deleli ambae pia ni Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani amesema ukaguzi huo utahusisha Madereva wenye madaraja C na E ambao wanaendesha Mabasi ya Abiria, Taxi na Magari ya Mizigo.
Kwa mujibu wa Kamishna Deleli, zoezi hilo linafanywa Nchini kote ambapo Dereva anatakiwa kuwasilisha Kituo cha Polisi Cheti cha Chuo alichosoma pamoja na Leseni yake ili kuhakikiwa kama ni halali na wana sifa.
Aidha, wenye madaraja A, B na D ukaguzi unaendelea kama kawaida lakini Dereva hatohitaji kuwa na Cheti cha Chuo alichosema Udereva.