Uhalali wa bunge la katiba kuja na rasimu mpya ya katiba

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,176
Reaction score
10,068
Wakuu JF,
Hivi kama Bunge la Katiba lina Mamlaka ya Kuja na Rasimu Mpya kabisa ya Katiba na kuifuta ile ya Tume ya Warioba hivi kulikuwa kuna uhalali gani wa Kuundwa kwa tume ya Warioba ?
Hivi Gharama zote iliyotumia tume ya Warioba Pamoja na weledi wao vije kumezwa kirahisi kabisa na Bunge la katiba lenye wabunge wengi wa CCM ambao wengine hawana hata Elimu ya Masuala ya Sheria na Katiba ?
Wa Tanzania naomba tuamke katika hili.
Gharama iliyotumia tume ya Warioba ni Bora ingeelekezwa kufanya Mambo mengine na Kazi yote ya Katiba kuchiwa Bunge la Katiba
 
Hivi ni wapi imesemwa kuwa Bunge la katiba litakuja na rasimu nyingine!!??
 
Kasema Bwana Mkubwa huko Mbeya jana. Kasema Bunge la Katiba, analoliteua yeye, "litaamua ni katiba ya namna gani iletwe kwa wananchi - wana madaraka makubwa na wataamua kwa niaba yetu sote."!!!!
 
Kitu kimoja cha msingi ambacho tunatakiwa kukijua ni kuwa Rasimu ya Katiba ( kama nilivyo isoma na kuielewa mimi) imejengwa katika misingi ya Serikali tatu. Kuanzia bunge la JMT (wabunge 75 tu), mambo ya Muungano 7, na mfumo wa Serikali ya JMT etc. Kwahiyo kama Serikali 3 hazitapitishwa maana yake kazi yote iliyofanwa na Tume ya Warioba haitakuwa na maana yoyote na Bunge itabidi lianze kutunga Katiba mpya itakayohusu Serikali mbili tu.
 
na hapa ndio patamu. je hilo bunge la katiba limezunguka lini kupata maoni ya wananchi mpaka wakae watuletee katiba tofauti na ile ya tume. ikumbukwe lwamba hii rasimu imepitiwa naabaraza nchi nzima ili kuiboresha leo bunge la katiba wakaikatae? bunge la katiba wanatakiwa kuiboresha rasim sio kuiburuga.
 
Kitu kimoja cha msingi ambacho tunatakiwa kukijua ni kuwa Rasimu ya Katiba ( kama nilivyo isoma na kuielewa mimi) imejengwa katika misingi ya Serikali tatu. Kuanzia bunge la JMT (wabunge 75 tu), mambo ya Muungano 7, na mfumo wa Serikali ya JMT etc. Kwahiyo kama Serikali 3 hazitapitishwa maana yake kazi yote iliyofanwa na Tume ya Warioba haitakuwa na maana yoyote na Bunge itabidi lianze kutunga Katiba mpya itakayohusu Serikali mbili tu.
Watafanya marekebisho ya katiba ya 1977 kwa kuingiza baadhi ya vipengele vya rasimu 2.
 
Ile ya kwanza ni 'rasimu tu"; mahali pa kuanzia na si mwisho. Bunge la Katiba ndio lenye madaraka ya kuandaa rasimu ya kupeleka kwa wananchi. Wakiamua kutupilia mbali kazi ya kina Warioba kisheria wana uwezo huo na wakaandika nyingine kabisa au wakafanyia marekebisho makubwa sana. Lakini nguvu ya mwisho ya kuamuka ni ipi inapita ni wananchi wapiga kura. Endapo zaidi tu ya asilimia hamsini wakikubali ndio imetoka hiyo!
 
Back
Top Bottom