Uhalisia wa Mifumo ya Uzalishaji/Utawala na Jamii Zetu kwa Mfano wa Ng'ombe

Uhalisia wa Mifumo ya Uzalishaji/Utawala na Jamii Zetu kwa Mfano wa Ng'ombe

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
26,021
Reaction score
79,710
Ujamaa (socialism): Una ng'ombe wawili, na unampa jirani yako mmoja.

Ukomunisti (communism): Una ng'ombe wawili, serikali inachukua wote wawili na inakupa maziwa.

Ufashisti (facism): Una ng'ombe wawili, serikali inachukua wote wawili na kukuuzia maziwa.

Unazi (nazism): Una ng'ombe wawili, serikali inawachukua wote kisha inakuua.

Ubepari (Capitalism): Una ng'ombe wawili majike, unauza moja na unanunua dume. Unazalisha ng'ombe wako wanakuwa wengi na uchumi wako unakuwa. Unawauza, unastaafu na unaishi kwa faida yako (unakula pensheni).

Ubepari Uliokomaa/Ubeberu (Modern Capitalism): Una ng'ombe wawili, unauza moja na unanunua dume. Unazalisha ng'ombe wako na unanunua ng'ombe wote wa majirani zako. Majirani unawaajiri wanakuwa wachungaji wako, unawalipa mshahara kidogo na wanakufa maskini.

Jamii ya Kimarekani: Una ng'ombe wawili, unauza mmoja na yule mwingine unamkamua atoe maziwa kama ng'ombe wanne. Kwa kukamuliwa zaidi ya uwezo wake anakufa. Unatafuta mshauri/mtaalamu wa mifugo ili akusaidie kujua chanzo cha kifo hiki.

Jamii ya Kifaransa: Una ng'ombe wawili, unaigomea Serikali kwa sababu unataka ng'ombe mwingine wawe watatu.

Jamii ya Kijerumani: Una ng'ombe wawili, unawabadilisha (genetic engineering) ili waishi miaka 100, wale chakula kidogo (mara moja kwa mwezi) na kujitibu wenyewe.

Jamii ya Kichina: Una ng'ombe wawili, unauza maziwa kwa Wachina wenzako na unazalisha maziwa feki kusafirisha na kuuza kwa nchi nyingine duniani.

Jamii ya Kiafrika: Una ng'ombe wawili, unakula wote siku moja na unaota/unajipa matumaini hewa kuwa wafadhili au jamii ya kimataifa watakupa wengine.

Unaenda kanisani na unatarajia ng'ombe wa miujiza. Unafunga siku 40 bila kula au kunywa ili ng'ombe washuke kutoka Mbinguni. Mwishowe Unakufa katika umasikini uliokithiri.

Akili ni muhimu.

Credit: Anonymous
 
Kuna nchi nyingine za Ulaya zimechanganya communism na capitalism.

Communism, unakatwa kodi lakini hulipii huduma za afya.

Capitalism, wenye pesa wanaruhusiwa kufungua biashara na kuzalisha ajira.
 
Kuna nchi nyingine za Ulaya zimechanganya communism na capitalism.

Communism, unakatwa kodi lakini hulipii huduma za afya.

Capitalism, wenye pesa wanaruhusiwa kufungua biashara na kuzalisha ajira.
Yes mixed economy naona ni nzuri pia.
 
Kuna nchi nyingine za Ulaya zimechanganya communism na capitalism.

Communism, unakatwa kodi lakini hulipii huduma za afya.

Capitalism, wenye pesa wanaruhusiwa kufungua biashara na kuzalisha ajira.
Hivi sisi Tanzania tuna practice mfumo gani?
 
Na uminywaji wa haki za binadamu. Leo Chifu Hangaya amesema sisi tuna demokrasia yetu na si lazima ifanane na wengine duniani.
Kwahiyo anamaanisha demokrasia haiwi defined universally? Kwamba demokrasia Marekani sio sawa na demokrasia Tanzania?
 
Back
Top Bottom