Tetesi: Uhamiaji Dar haitoi passport kisa hakuna mtandao wa TTCL. Ukitoa kitu kidogo unapatiwa kwa siri sana

Tetesi: Uhamiaji Dar haitoi passport kisa hakuna mtandao wa TTCL. Ukitoa kitu kidogo unapatiwa kwa siri sana

Unko T

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
200
Reaction score
266
Tangu juma lililopita nimekuwa nikifuatilia passport yangu idara ya uhamiaji Dar es Salaam, iliyopo ndini ya ofisi za Mambo ya Ndani ya Nchi. Napewa jibu rahisi sana na afisa aliyekaa nje ya mlango wa kuingilia ofisi hizo, "Hakuna network ya TTCL hivyo hatuwezi kuona passport yako"

Nikajiuliza inamaana kwa wiki nzima hakuna aliyefikiria njia mbadala ya kuhudumia wateja/watanzania hata kama hiyo "network" ya TTCL haipo?

MAZINGIRA YA RUSHWA
Kuna mchezo nimeshuhudia, afisa anataka umuombe namba, um'pigie, akuulize majina yako matatu, UTOE RUSHWA, akutafutie passport yako ambayo utapewa kwa siri na wasaidizi/wahudumu wa usafi wa ofisi zao wenye tisheti/formsix/polo za blue zenye logo ya M.

Tafadhali wahusika rudisheni huduma ya kutoa passport za wateja tenu na ouache kutengeneza mazingira ya RUSHWA eti hakuna "network" ya TTCL. Watu gani msiokuwa wabunifu kutatua changamoto za mnaowahudumia?

Naomba TAKUKURU wafanyie uchunguzi madhila haya kwa maslahi mapana ya Tanzania.
 
Unko T,

Rushwa siku hizi huko kwenye ofisi za Serikali imezagaa sana hata hawaogopi tena!! Mpaka kwenye mabaraza ya kata shauri halizikilizwi mpaka mshitaki atoe chochote eti wanaita fedha ya kufungulia file lakini haina risiti!!! Magufuli vita hii inataka mkakati mpya!!
 
Katika Watu Wenye Njaa Ukiondoa Walimu police wanafata uhamiaji duh awa jamaa wamekula pesa zangu kibao sana yaani wana njaa balaa
 
Unko T,

Rushwa siku hizi huko kwenye ofisi za Serikali imezagaa sana hata hawaogopi tena!! Mpaka kwenye mabaraza ya kata shauri halizikilizwi mpaka mshitaki atoe chochote eti wanaita fedha ya kufungulia file lakini haina risiti!!! Magufuli vita hii inataka mkakati mpya!!

Mjinga ndiye hutoa rushwa.
 
Ungekua unamjua mtu akakusaidia kwa malipo ungesema una connection au network. Huna mtu imekua rushwa!!
 
Si usubiri tu mkuu mpaka TTCL ikae sawa, au una haraka sana na hii corona unaenda wapi?
 
Back
Top Bottom