DOKEZO Uhamiaji Kibaha changamoto ni nyingi sana na hakuna hatua zinazochukuliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Serikali na vyombo husika vinapaswa kuliangalia hili tatizo la kukwama kwa maombi ya passport/hati za kusafiria ni mwaka sasa wananchi hawajapa passport za umeme na server zikidaiwa kuwa ni sababu za kukwamisha hayo maombi

Wizara nyeti kama uhamiaji inawezekanaje kukaa ndani ya mwaka mzima bila ya kutoa huduma na raia washalipa pesa za passport na kama mfumo wa umeme server ni mbovu wananchi warejeshewe pesa zao serikali hatuna pakwenda hatuna pakulilia.

Tunaomba pesa zetu zirejeshwe, tukienda uhamiaji kudai pesa zetu tunatishiwa amani na lugha chafu tunatamkiwa hii inauma sana.

Nimejaribu kupost hii mara kadhaa nikidhani kuna hatua yeyote inaweza chukuliwa watu wanaendelewa kuibiwa pesa zao Uhamiaji Kibaha Serikali iingilie kati.

Pia soma ~ Bashungwa Atoa Miezi Miwili kwa NIDA, Vitambulisho Milioni 1.2 Vilivyotengenezwa Kuwafikia Wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…