Pre GE2025 Uhamiaji: Mgeni Aliyeomba Uraia wa Tanzania anaweza kuwa Mbunge au Waziri ila haruhusiwi kuwa Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Akishafika kwenye nafasi za juu kabisa za Uongozi sidhani kama atataka kuisaliti Nchi iliyompa hayo mema ilihali anajua yeye hapo ndipo atakapoishi maisha yake yote mpaka kifo kimkute !
Huku Barani kwetu watu hawawapendi watu wao kihivyo unavyojaribu kufikiria. !
Angalia baadhi yao huwa wanaziibia Nchi zao za mababu na mabibi zao na kuziweka pesa zao Ughaibuni !!
Iko vile watu wanataka kujilimbikizia sio kuzisaliti Nchi wanazoishi na vizazi vyao !!
Labda wale wenye nyadhifa za chini na renki za chini chini sio zile za juu !!
 
Rais gani huyo? Samia anamjua? CCM wanamjua? Nani alimpa Urais? Nani alimpitisha kugombea Urais?
Ndio maana watu wanataka CCM mtoke madarakani kama mnakiri kutuletea mgeni kuwa Rais basi hamfai kuongoza nchi!
Magufuli alikuwa Mrundi haswa
 
Stupidful
 
Kwa hiyo kuwa Naibu Waziri Mkuu ni sawa? Kwa sababu amesema kuwa endapo wakiomba uraia, ni vizuri autangazie umma Naibu Waziri Mkuu na hawa wengine wanaotajwa, kama waliwahi kuomba uraia wa Tanzania, waliomba lini na walipewa lini.
Nasibu Waziri Mkuu yaan unamaanisha Dotto Biteko Waziri wa Nishati
 
Sawa lakini,
vip kuhusu uzalendo,
Raia mhamiaji atakuwa Mzalendo wa nchi aliyohamia zaidi ya raia Mzawa?
Wale tunaoamini kuwa ni raia wazawa kabisa kabisa ndio hao hao wakwapuaji wakuu wa mali za Nchi na kujilimbikizia mimali kibao kwa kuingia mikataba ya ajabu ajabu na Nchi za Ughaibuni !!

Nchi zote za Africa zinapitia hii Shida !!
 
Nchi imejaa wahuni Kila jambo linapindishwa ili waendelee kuiba,hiyo Kwa urefu wa kamba hadi 2030 nchi itabaki mabua tu.
 
Wale tunaoamini kuwa ni raia wazawa kabisa kabisa ndio hao hao wakwapuaji wakuu wa mali za Nchi na kujilimbikizia mimali kibao kwa kuingia mikataba ya ajabu ajabu na Nchi za Ughaibuni !!

Nchi zote za Africa zinapitia hii Shida !!
Wazawa wataiibia hii nchi.

Ila wageni ambao ni ma puppeti wa serikali zao wata iangamiza hii nchi.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…