Ndugu yangu.
Ukisoma Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 [Public Service Act No. 8 of 2002] pamoja na marekebisho yake Na. 9 ya mwaka 2007, na Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 [Public Service Regulation of 2003] pamoja na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la tatu la mwaka 2009 [The Standing Orders, third Edition of 2009]. Aidha hata ukisoma Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 [The Employment and Labour Relation Act No. 6 of 2004] na Kanuni zake za mwaka 2007 [Rule of Employment and Labour Relation of 2007] Hakuna sehemu inayosema mtumishi wa Umma au Binafsi atahamishwa kwa adhabu baada ya kufanya makosa.
kwa maneno mengine UHAMISHO WA ADHABU ULISHAFUTWA.
Nipatie taarifa kamili za mwajiri wake huyo mtumishi kama ni wa Umma kama ni binafsi namshauri aende kwenye vyama vya kutetea watumishi.
E-Mail yangu ni:
nkembanyi74@yahoo.co.uk