Uhamisho wa watumishi wa umma

Uhamisho wa watumishi wa umma

Maria Nyedetse

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2021
Posts
661
Reaction score
1,501
Salam ndugu zangu wana jamvi

Naomba kuuliza swali jepesi, umewahi kutokewa au kusikia ndugu yako au Jamaa yako mtumishi WA Serikali anapata uhamishi kutoka sehemu moja ama nyingine lakini kashindwa kufanikiwa kuhama kwa sababu ya kutopata barua kutoka kwa mwajiri wake wa sasa??

Kama hujawahi kusikia basi scenarios hizi ni za kawaida sana kwenye ofisi za umma.

Kuna mambo huwa najiuliza...
1. Katibu Mkuu Utumishi au OR-TAMISEMI anapoandika barua kumhamisha Mtumishi kutoka eneo moja kwenda jingine HUWA ANARUSHA JIWE ANGANI BILA KUWA NA SHABAHA MAALUM?? kama siyo inakuwaje barua inaweza kuwa blocked katikati, mtumishi asihame naye hajui?

2. Je kiutumishi watumishi wa chini yake wanaweza kuamua kuitekeleza barua husika au vinginevyoo?

3. Je mtumishi hana haki ya kujua kuwa amehamishwa mpaka ategemee MERCY ya mwajiri wake wa sasa?

4. Hakuna jitihada zinazofanyika kujua ni watumishi wangapi wamereport kwenye vituo vyao baada ya kuhama? Na kama hajarepoti hatua gani zinafanyika kuhakikisha mtumishi husika anahama?

Kutokuwepo kwa utaratibu mzuri na wa wazi NDIYO CHANZO CHA KUWA NA VISHOKA OFISI YA OR TAMISI NA UTUMISHI kwa sababu uhamisho kwa watumishi limekuwa jambo lisilo na uwazi na kushughulikia kwa njia nzuri.

Kwa nini pasiwepo na utartibu wa mtumishi kuwa notified either online au vinginevyoo kuwa umehamishiwa eneo flani na barua yako imetumwa kwa mwajiri wako wa sasa ili kuleta uwazi.

Mtumishi mwingine unakuta amekaa kwenye kituo kimoja zaidi ya miaka 10, anapopata fursa ya kupata uzoefu mpya sehemu nyingine kwa nini asiruhusiwe na mwajiri wake wa sasa?

Wakati mwingine nafasi mpya, mazingira mapya huamsha ari na moyo wa kujifunza na kufanya kazi kwa bidii na kinyume chake mazingira ya kazi hugeuka kama kifungo na kumfanya mtumishi afanye kazi kwa mazoea na kukosa MORALI!!!

Nadhani kwenye ulimwengu wa kidigitali suala la uhamisho wa watumishi linapofikia amepewa ruhusa, kuhamishwa kutoka eneo hadi jingine NAKALA YA BARUA YAKE YA UHAMISHO IWE ATTACHED KWENYE ACCOUNT YAKE YA UTUMISI AU HATA EMAIL BINAFSI kuongeza UWAZI na kuondoa mianya ya RUSHWA NA UKIRITIMBA.


Aidha waajiri WARETAIN WATUMISHI kwa INCENTIVES na GRIPS, HOOKS AND CROOKS.......

Mwisho; Napongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kuajiri [watumishi walioajiriwa katika kipindi cha miaka 4 ni wengi kuliko watumishi wote walioqjiriwa katika kipindi cha miaka 5 ya serikali ya awamu ya 5], kuboresha maslqhi ya watumishi na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi!!! KONGOLE MHE. DR. SAMIA SULUHU HASSAN.

Aidha, nashauri kwa sababu ya changamoto kubwa za ajira, baadhi ya maeneo kama elimu, afya [isipokuwa eneo la ubobezi au kibingwa] watumishi waanze kuajiriwa kwa mikataba ili kuleta ushindani, ubunifu na uwajibikaji kwenye utumishi wa UMMA. Permanent and Pensionable badala ya kuwa incentive ya kuwajibika, imekuwa chanzo cha watumishi wengi kufanya kazi kwa mazoea. Kwanini hospitali binafsi au shule binafsi watumishi wawe so punctual na motivated kutoa huduma hata kama mishahara ni midogo [zile startups] lakini kwenye facilities [baadhi] za umma watoa huduma wanafanya hivyo kwa mazoea? Ni kwa sababu ana uhakika wa mshara na posho...

Kuna Akina TEMESA, TBA, n.k huwezi kuulinganisha na kampuni binafsi.....

Kwa sabu wana uhakika na mishahara na posho...
 
Pole, changamoto za uhamisho haziwezi kuisha kirahisi. Kwasasa kuna ESS ambayo ingesaidia kama sio kurahisisha ila wahusika wapo tu ofisini hawafuatilii habari zilizopo kwenye mfumo.
 
Kuhama ni jambo gumu kuliko kupata ajira mpya.
 
Kuna wengine unapata uhamisho, wenyewe wanakwambia hawajapewa maelekezo.
Huwa inanikera sana Sasa hutaki nihame kivipi Tena dar kwenda mkoani lakini mtu anaumia ukifuatilia utaambiwa Kuna uchache wa watumishi kwanini wasingeweka utaratibu sekta zote serikalini wawe na uwezo wa kubadilishana sehemu ya kufanyika kazi kama ilivyo kwa waalimu.
 
Back
Top Bottom