Ushauri mzuri huu
Sasa ninaamini kuwa serikali yetu ni sikivu na pia watendaji wake wanapitia mitandao ya Jamii na kuyafanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wananchi hasa humu Jamii forum! Juzi kulikuwa na uzi juu ya uhalibifu wa mazingira ya mto Ndumbwi kwa wavamizi kuzungusha ukuta kwenye open space ambayo iko ukingoni kabisa mwa mto; leo Katika pita pita zangu nimeona ukuta ule uliojengwa umepigwa "X" na maandishi yanayo someka BOMOA HARAKA. Hata hivyo inaelekea kulikuwa na jitihada za kufuta stop order hiyo kwani mafundi walionekana kuchapia cement ili maandishi yasionekane.
Inaelekea hawa wavamizi ni watu wanaojiweza kifedha hivyo wanaweza kukaidi amri hiyo ya kusitisha ujenzi wa uzio; kimsingi NEMC au Manispaa ya Kinondoni wana kila sababu ya kumpiga faini huyo anayejenga , na kuvunja ule uzio na kuhakikisha mvamizi huyo analipa gharama zote za uvunjaji!! Hilo litakuwa fundisho tosha kwa wavunjaji sheria za mazingira.
Serikali imelala, inawaza kumsulubu @MBOWE
Serikali ya kiboya sana hii, yaani diwani tu kawaweka mfukoni NEMC na wizara nzima, shenzi taipusi pwayipwayiNadhani hawa wavamizi wanaamini kwamba serikali imelala kwani kasi wanayotumia kujenga uzio kuzunguka ile open space sio ya kawaida. Uvamizi huu bila ya shaka una mkono wa diwani wa Kawe ambae ni mtoto wa kiume wa marehemu mama Rwakatare kwani haingii akilini kuwa huyu diwani ambae anaishi kwenye nyumba jirani na hiyo open space asijue kile kinachoendelea mbele ya nyumba yao.
Serikali haina budi kumuuliza diwani huyo nani anahusika na ujenzi huo na akipatikana apewe adhabu ya mfano ikiwa ni pamoja na kuubomoa huo uzio uliojengwa kinyume na sheria. Kama huyu diwani angekuwa muadilifu bila ya shaka ujenzi huu wala usingeanza!! Manispaa ya Kinondoni wakisaidiwa na wizara ya mazingira ni lazima wachukue hatua za haraka kuzuia uharibifu unaofanywa kwenye lile eneo.
Haguswi mtu paleLeo nimeona kwenye gazette la Nipashe naibu Waziri wa mazingira na Muungano ameamuru kuwa NEMC iwaadabishe wale wote waliojenga kinyume na sheria pale Salander bridge!! Hilo agizo kwa NEMC ni lazima liwe kwa wale wote nchi nzima waliokiuka sheria ya mazingira; wakiwemo wale waliojenga Mbezi beach pale mto Ndumbwi unapoingia Bahari ya Hindi!!! Kuhamia Dodoma hakuna maana kuwa serikali haipo tena Dar es salaam.!!!
Nchi hii mambo yanafanyikaga kwa mupe murukeMawaziri wawili Azzan Zungu wa mazingira na William Lukuvi wa Ardhi are accountable kwa uharibifu unaotokea kule mto Ndumbwi unapoingia baharini [ Mbezi Beach] bila kuchukua hatua. Magufuli anahitaji watu wanaomsaidia kazi kuendesha nchi kufuatana na sheria, hivyo fanyeni kazi zenu msimgoje mpaka yeye aje ndio muanze kushuhurika!!
Nchi hii mambo yanafanyikaga kwa mupe muruke
Weka location tupajueni wapi hasa