Uhasama wa KIANJA na KARAGWE

Uhasama wa KIANJA na KARAGWE

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,174
Reaction score
16,794
UHASAMA WA KIANJA NA KARAGWE

Wakati wa utawala wa kijerumani ndani ya buhaya(bukoba),Omukama Kahigi wa Kianja alikuwa na nguvu sana kwa maana yeye aliwakaribisha Wajerumani katika utawala wake.

Wakati huo aliyekuwa mukama wa Kiziba,alikuwa no omukama Mutahangarwa na karagwe alikuwa ni Omukama Ntare.

Abakama wa karagwe na Kianja wote walikuwa ni ukoo wa Abahinda,lakini waliingia katika ugomvi wa ukoo na utawala kwa maana Omukama Kahigi alishirikiana na wajerumani hivyo akaomba msaada wa kumuondoa katika utawala, Omukama Ntare alikuwa na mahusiano ya karibu zaidi na Kabaka wa Buganda,hivyo Kahigi aliwaambia Wajerumani kuwa Omukama Ntare anashirikiana na Kabaka na hivyo atapata msaada kutoka kwa waingereza ambao walikuwa wakiitawala Uganda,Hivyo omukama Ntare alionekana kama msaliti kwa Wajerumani.

Usaliti huo ni kutokana na vuguvugu la vita vya dunia vya kwanza,Mjerumani hakupatana na mwingereza,hivyo Omukama Ntare kushirikiana na Waingereza ilikuwa ni kuzidisha chuki na hasira za Wajerumani (lakini Ntare yeye alikuwa karibu zaidi na Kabaka wa Buganda na sio Waingereza) japo ilichukuliwa kwa mtizamo huo.

Hakika Wajerumani walimkamata Omukama Ntare na Kumnyonga hadharani,na kisha Omukama Kahigi akapewa mamlaka ya kuitawala Karagwe,hivyo akawa mukama wa Kihanja na Karagwe,. Baada ya Kahigi kuona kuwa watu wa karagwe wamemchukia sana na kutompa heshima ya utawala, aliamua kumuweka shemeji yake aliyejulikana kwa jina la Kiobya ili awe msimamizi au mtawala kwa niaba yake huko karagwe.

Huyu Kiobya alikuwa ni Ukoo wa Abarwani,hivyo yeye alilipoti taarifa zote kwa Kahigi,suala hili la Kiobya kuwa Omukama Karagwe,liliwachukiza sana Watu wa karagwe na kuonekana kama ni dharau na fedheha kwa wao kutawaliwa na ukoo wa Abarwani ambao ilikuwa ni mwiko kuingia katika hekalu la utawala.

Tangu hapo ikawa ni chuki kati ya Karagwe na Kianja na ndipo Watu wa KARAGWE walipoanza kujitenga na kujitoa katika Buhaya Union na kuanza kujitegemea.

Mnamo 15 June 1915,Waingereza kutoka Uganda waliivamia Bukoba ikiwa ni vita vya kwanza vya dunia na Wajerumani wakawazuiya Abakama wasipambane vita dhidi ya Waingereza, na mnamo 1916 Wajerumani waliondoka Buboka na kurudi Ujerumani wakiliacha koloni kwa mwingereza.

Baada ya Waingereza kuanza utawala wao buhaya, Walimsimika mtoto wa Omukama Ntare wa karagwe kuwa Omukama, Kijana huyo alikuwa ni Omukama Daud Rumanyika.Kahigi wa Kianja hakuwa tayari kushirikiana na Waingereza na hivyo alijinyonga yeye mwenyewe na mwili wake ulizikwa Buchwankwanzi, asingezikwa katika ngome yake kwa kuwa alijinyonga yeye mwenyewe hivyo ilikuwa ni mkosi na laana.

Omukama Kahigi ndiye baba yake na omukama Rugomola lwa Mahe.

Share na wengine wasome

Katika picha ni Omukama Kahigi wa kihanja.

dbaenganzi@gmail.com
 
Picha haionekani mkuu
 
Kuna hadithi kua;karagwe ilifua chuma kabla.ya Ulaya je.nikweli? Kanazi haiku's na Mkama.
 
Back
Top Bottom