Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Mechi ya Leo kati ya Tanzania na Kenya imelipua pia chachu ya uhasama ambao unaletwa na siasa kutokana na kauli mbalimbali za viongizi, wasanii na raia wa kawaida.
Je, uhasama huu ndani ya mpira unaweza kuleta mashamshamu kama yale ya USA ilipokutana na Iran world Cup?
Nadhani hii itakuwa zaidi maana ukiacha kauli za kina Jaguar na wabunge wetu, kuna kingine hapo.
Victor Wanyama anayekipiga EPL alitembelea Tanzania na kupongezwa kwa kuleta mashamsham katika Ndondo Cup mwaka jana,. Hali hiyo iliifanya meya mmoja wa munispal kumpa Wanyama mtaa.
Kilichotokea kwa vile meya huyo hakuwa wa CCM basi Makonda alifuta jina la mtaa huo kibabe na kumfedhehesha Wanyama.
Leo Wanyama anaongoza mashambulizi ya Harambee na Makonda anaongoza washabiki wa Taifa stars, hapo sasa ndio mtanange nani ainamishe kichwa kwa fadhaa?
Je ni Makonda na Taifa kwa jumla au Wanyama na Kenya yake?
Hii ni zaidi ya US na Iran.
Pamoja na Makonda kuingia na kutuharibia mood, bado tunaomba Mungu aibariki Stars.