Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

kwan kati ya mmasai wa tz na mmasai wa kenya vs mmakonde yupi ndugu zaid ? ccmu inajaa wajinga siku hz

hoja za Lissu zipo wazi kwann mtanganyika hanaonekana raia daraj la pili kule zenji ?

ukute wewe ni mtanganyika ila ccmu wamekujaza ujinga
Ndo nasema tunabaguana kwa mipaka iliyowekwa na wakoloni 1800, hadi leo tumeingangania tu, watu kama lissu anazungumzia mipaka ya kikoloni hadi leo na mbaya zaidi anaishi hukohuko kwa wakoloni, kuna shida gani mpemba kutawala tanganyika, kwanza tunataka eac iwe na raisi mmoja, tuachane na viserikari vidogovidogo, juzi mseveni alikuwa anatetea maslahi ya wakenya.
 
Wewe unaona upande mmoja tu je vipi kelele za wazanzibar hauzisikii tena wakiwemo viongozi wa ccm, act na wananchi wote wa Zanzibar au wewe ni mnufaika wa dhuluma kwamba siyo mwumini wa haki?
 
Wewe unaona upande mmoja tu je vipi kelele za wazanzibar hauzisikii tena wakiwemo viongozi wa ccm, act na wananchi wote wa Zanzibar au wewe ni mnufaika wa dhuluma kwamba siyo mwumini wa haki?
Hizo ni kelele za jussa, hakuna mpemba aliyefuatwa kuja tanganyika
 
Hivi tukisema EAC tuwe na raisi mmoja, itakuwaje kuhusu Zanzibar? Kwa sababu Zanzibar ni part ya Tanzania katika EAC, haina uanachama wake wa EAC. Unajua kwa jinsi tunavyoendekeza mambo, hilo linaweza kufanya Tanzania ikatae uwepo wa East African Federation au States chini ya raisi mmoja?

Kwa jinsi Zanzibar wanavyopenda kujiona ni big fish in a small pond, japo ni small fish, itakuwa ni mtihani mwingine!
 
kwanza tuliumia sana ile kufukuzwa na kunyanyaswa masai, ati hawaendani na utamaduni wa kizanzibari, upi? wazanzibar wana utamaduni upi ulio tofauti na wa wabantu wengine, na wamasai hao wazungu wanawapenda sana kiutalii na nchi yenu inapumulia utalii tu. utamaduni gani huo wa kizanzibari au mnamaanisha utamaduni wa kipemba? ni kweli kama mambo yale ya kipemba sisi wabara hatuwezi kuufuata, kaeni hao hukohuko.
 
Mkuu Mbogi , Kwanza naheshimu mawazo yako, sijapenda unavyoniita mpotoshaji!. Sii wengi wanajua tofauti ya mkataba contract na makubaliano, agreement. Mkataba ni legal binding, makubaliano sio legal binding.

Watanzania wameaminishwa zile Articles of Union ni mkataba wa muungano, ukweli ule sio mkataba bali ni makubaliano tuu!.

Kinachofanya Articles of the Union zisiwe mkataba bali ni makubaliano tuu, ni kwasababu zimekosa moja ya sifa kuu za mkataba, kwenye kitu kinachoitwa privity, kila mkataba lazima uwe na kipengele cha kuuvunja mkataba, Articles of Union hazina kipengele cha kuuvunja muungano!. Take it from me, it's muungano for life!. Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?

Tanzania tuna bahati sana sasa, tuna rais aliyeruhusu tuujadili muungano. Enzi za Nyerere, ilikuwa ni taboo topic, kitendo cha kuwaza tuu kuuvunja muungano ni uhaini!. "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
P
 
Bro Umezungumza kama dikteta hujatoa suluhisho nini kifanyike kutatua KERO ambazo ndio msingi wa hoja za muungano na mara nyini wanasiasa zaidi ni maslahi sio ufumbuzi wa kudumu kwa nini iwe chako chetu na chetu chetu?
Solution ya kumaliza kero zote za muungano naizungumza humu, kila siku, nayo ni moja tuu, serikali moja!.
2014 - Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
- Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?

- Pongezi za Miaka 60 ya Muungano: Twende Kwenye Muungano Kamili wa Ukweli wa Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja? Kero Zote za Muungano Zitayeyuka!
P
 
Pascal, kwa hiyo unataka kusema muungano huu ni makubaliano yahiari kwamba hauwezi kivunjwa kwa kuwa tu hauna kipengele cha kimkataba?

Kama ndivyo (yaani hiari) unapata nguvu gani za kutuaminisha kuwa Muungano wa hiari lazima uwe wa kudumu milele au mnataka tuje kufikia kuwa kama Urusi na Ukraine. Ni vema kwa sasa ukaendelea kuelimisha tuwe na muunfo sahihi usio na manunguniko kwa pande husika ili kuepuka mtafuruku huko mbele. Leo unaona kama haiwezekani kutokea vurugu kwa unyonge tu wa wanzanzibar au watnganyika ila ujue utafika muda na kizazi tofauti.
 
Hivi Tanzania bara ndio wapi huko?

Mimi ninavyojua Kuna Tanganyika na Zanzibar.
 
Mkuu unajifariji.
Iwe ni makubaliano iwe ni mkataba as long as imehusisha pande mbili hapo tu tayari ni shida.
Tatizo ni undumi lakuwili. Labda Tanganyika iendelee kufaidi Muungano huu milele ila ikifika siku Tanganyika hainufaiki hapo ndipo zilipo funguo za Muungano huu.

Funguo zengine ziko kwa Kura ya Maoni ya pande mbili za Muungano ikiwa zitabariki aina ya Muungano unaohitajika au hata kutokuwepo muungano wenyewe.

Mkuu wewe unadhihirisha tu kile kilichopo kwenye nafsi za malengo ya Tanganyika kuidhibiti Zanzibar milele na ndipo mara zote unaishia kufanya "Conclusion" Muungano utadumu milele na hauvunjiki.

Maana tayari kwa namna mlivyouzonga Muungano wenyewe ni as if una uhakika sasda haiwezekani kuvunjwa tena.
Kumbuka tu vile vile kuna Sheria za kimataifa na elewa tu kwamba Zanzibar ni Nchi yenye mipaka yake.
Wakati ni Mwalimu mzuri.

Kishada
 
Wazanzibari walipodai Zanzibar yao, hakuna madhara makuwa yaliyojitokeza labda tu kule kuchafuka kwa hali ya kisiasa; leo waTanganyika wakidai Tanganyika yao eti kutatokea madhara makubwa!
Ninachoona ni kuwa Watanganyika walikuwa wamelala sasa wanaamshwa kudai Tanganyika yao, wapewe kama Wazanzibari walivyopewa Zanzibar yao.
Utasikia Mzanzobari anasema 'tunajitambua' na Katiba yao inawatambua kuwa wao ni Wazanzibari lakini Watanganyika hawajajitambua na Katiba haimyambui Mtanganyika bali inamchanganya na Mzanzibari kuwa wote ni Watanzania- Shida iko hapo.
Sasa Wazanzibari wanasema wamemezwa na Tanganyika, na Watanganyika wanasema wamemezwa na Tanzania maana yaye wote hawaridhiki na hali ilivyo - wote wasikilizwe ili muafaka mpya upatikane.
 
Na hatuelezwi ni kero zipi zimetatuliwa na zimetatuliwaje - isije kuwa zimetatuliwa kwa gharama ya Tanganyika! Uwazi ni muhimu sana
 
Hujui au umejisahaulisha kuwa katika Muungano wetu kimekufa kimoja tu, kingine kikabaki; katika hali hiyo hoja yako ya chemical reaction to form a compound si sahihi. Kwa mantiki hayo hayo basi hii ni mixture.
 
Hapana kwa mara ya kwanza nakupinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…