Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Uholanzi nayo imeamua kusitisha matumizi ya chanjo ya corona ya Oxford-AstraZeneca kwa kuhofia kuwa na madhara.Serikali ya Uholanzi imeamua kuchukua hatua hiyo mpaka Machi 29 ili kuchukua tahadhari.
Awali Jamuhuri ya Ireland ilichukua uamuzi huohuo kwa kuhofia hatari ya watu kuganda damu baada ya kupata chanjo hiyo nchini Norway.
Lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) hakuna uhusiano wowote baina ya chanjo hiyo na hatari ya watu kuganda damu.
Shirika la madawa la Muungano wa Ulaya(EMA) lilisema awali kwamba hakuna dalili kwamba chanjo hiyo inasababisha kugada kwa damu mwilini, likiongeza kuwa ni "faida ambayo zinaendelea kuwa kubwa kuliko hatari zake.
Denmark, Norway, Bulgaria, Iceland na Thailand pia wamesitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca.