Ni kweli kabisa NEC au sijui ndio hii tume ya Uchaguzi ya Taifa na matawi yote ni wabaya sana sana .
Kama utafatilia utaona kumejitokeza uwekaji pingamizi na uwekaji huu unatumika katika kuisafishia njia CCM kwa pale ambapo wana wasiwasi wa ushindi ,hivyo huwaengua wapinzani kwa kutumia pingamizi, mtindo uliotumika safari hii ni kuihakikishia CCM inapata ushindi wa chee mapema ,usitegemee kuwa mgombea wa CCM ataondolewa kwa kutumia pingamizi ,hata pingamizi hilo liwe na uwazi kiasi gani,si tumeona wameweza kuwalinda mafisadi watashindwa kwa wagombea ?? Ila wapinzani hata kama pingamizi halina kichwa wala miguu litatumika kikamilifu ili kumuondoa au kuwaondoa wapinzani ,NEC (Tume ya uchaguzi) inatumika kuinyanyua ccm. Ni uhuni tu .