Uhuru hana tena Moral Authority ya kuwa Rais Wa Kenya..

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Mimi nikiri wazi kuwa nilikuwa shabiki mkuu wa Uhuru Kenyatta kwa sababu ya mapenzi ya democrasia lakini kwa kinachoendelea kenya kwa sasa siwezi kuwa mnafiki kuendelea kushabikia upuuzi unaofanywa na serikali yake hakika sijui ni kwa kushauliwa au ni kwa makusudi .

Ingawa sijawai kuwa shabiki pia wa Siasa za Raila Odinga lakini kwa yanayoendelea kenya mwenye unafuu ni Raila kuliko Uhuru ..

Serikali kupitia police wanafanya mauaji ya kikabila its so sad sana watu zaidi ya 30 wote wa kabila la mgombea wa upinzani?..

Sasa hivi huyu mama wa IEBC kajiuzulu kwa sababu ya kutishiwa maisha na watu wa serikali kwa kweli ni aibu kwa mfuasi makini wa siasa za kidemocrasia kuendelea kumuunga mkono Mtu wa namna hii...

Hapa bado sijaweka mauaji ya Msando na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi kabla ya Matiangi kiukweli ni laana ...

Uhuru kama alifanya haya kwa kujua basi hatakiwi kuendelea kuwa rais wa kenya taifa linalojipambanua ni taifa la democrasia namshauri ajiuzulu au awafukuze kazi waliomshauri kufanya uhalifu huo wa kinyama bado sioni nafasi yake tena kama rais mwenye heshima east africa .
 
Siasa za kenya huzijui kabisa.

Musando aliuawa na mapenzi nje ya ndoa siyo na Uhuru.

Huyu Mama Roseline Akombe na IEBC Chair ni NASA moles sasa ulitegemea nini?

Mauaji hakuna aliyethibitisha hadi leo upande upi wahusika mengine ni wewe wayapika
 
Kuna bango la waziri wake mmoja kuhitajika akajieleze un
 
hata r hujui matumiz yake
 
Kenya kuuliwa ni jambo rahisi kama kwenda msalani. Next ni RAO mchezo uishe
 
Ni rahisi sana kuahidi kuwatumikia wakenya ukiwa kwenye kampeini ili upewe kura. But, once umeingia pale ikulu, akili huharibika kwa sababu unakutana na mabo mingi na unatamani uyamalize yote kwa mara moja.
Uhuru was very very good in the beginning but as time went by, akaharibikiwa. He is not in the right path. Labda ni ile majani wanasema anakula imemharibu
 
Mangatara! Yeye na Ruto walijaza marafiki, girlfriends (eg.Waiguru) kwenye cabinet wakakosa nguvu ya kuwabana hao CS. Hatimaye Rushwa imeongezeka kila kona, SGR wameenda kuleta treni sawa na la TAZARA miaka ya 1970
 
Maafisa wa iebc wanatishiwa maisha kwa ngome za NASA (kisumu, homa bay,vihiga) tuache kuekeleaga serikali kwa kila kitu.......Leo mama flani kisumu amepigwa kwa sababu ya kueka tents zitakazo tumika na iebc kuwafundishia maafisa walioalikwa na iebc..na alikua akiongoza watu kumpiga mama huyu na kumharibia mali yake ni senata wa kisumu...na si propaganda tazama news za saa moja..so tunajua nani wanawatishia maafisa wa iebc acha side shows
 
Mwathadan huko western wafanye nn zaid baada ya kuwapoka keki ya taifa kwa miaka zaid ya 50?
 
Siasa za kenya huzijui kabisa.

Musando aliuawa na mapenzi nje ya ndoa siyo na Uhuru.

Huyu Mama Roseline Akombe na IEBC Chair ni NASA moles sasa ulitegemea nini?

Mauaji hakuna aliyethibitisha hadi leo upande upi wahusika mengine ni wewe wayapika

Wewe ndie mgeni wa siasa za kenya
na huijui historia ya kenya
nahisi bado ni kitoto sana!

Mauaji ya kikabila Kenya hayajaanza leo wala jana
Sitaki kutaja majina ya watu
Yupo kiongozi aliye kuwa Kabila pinzani na la huyu Rais alipigwa Risasi akitoka kwenye ATM miaka hiyo na kuleta Kasheshe Kenya nzima
watu waliuana vibaya .
Tatizo kenya ni Kuona Aina moja ya Kabila ndio Wamiliki halali wa nchi ya Kenya
Mkosoaji mkubwa wa Uhuru Jaccobo Alipigwa Risasi na kuuliwa Majuzi tu hapo
 
Leteni mbwembwe muelewe mtaumia ninyi
 
Yote haya uamuzi wa mahakama kutengua matokeondio chanzo..
 
Mleta mada huwa napenda sana hoja zako haswa kule kwenye jukwa la siasa za Watanzania maana mara nyingi huwa hauegemei upande wowote, sio kama wale mamluki tumezoea humu. Nakumbuka siku umempelekesha sana waziri wenu Mwigulu hadi akafungua uzi kujitetea humu JF.

Sasa kwenye kauli zako leo, japo kuna maeneo upo sahihi lakini mengine naona kama utakua aidha hujatumia muda wako kudadisi ipasavyo.
- Majina ya watu waliouawa yalidhihirisha sio watu wa kabila moja pekee, humo niliona hata majina ya Wakikuyu kabila la rais Uhuru.
- Ni kweli waliouawa wengi ni Wajauo, kabila la Raila, japo pia kuna uchunguzi unafanywa ieleweke waliuawa kivipi, maana kuna tetesi haya mabunduki yanayoibuka kutoka kwa mfadhili wa upinzani kuna yaliyotumika kwenye mauaji ya hao raia. Swali ambalo limezua utata ni kwamba, ni polisi yupi huyo aliyediriki kupiga watoto risasi, kisa kama hicho inafahamika lazima kitaibua hisia kali dhidi ya serikali, hivyo hilo suala linaangaliwa kwa jicho la tatu na kufanyiwa uchunguzi.

- Huyo kamishna mdada aliyejiuzuru ameeleza kwamba maisha yake yalikua hatarini kwa vitisho, kitu kinachofahamika ni kwamba kufikia hapo, wahudumu wa tume wanaogopa sana upinzani zaidi ya serikali. Kwa mtumishi yeyote kuthubutu kufanikisha zoezi hilo kwenye ngome ya upinzani ni kama kujitakia kifo. Huyo dada ameeleza hali ilivyo mbaya baada ya yeye kwenda huko kwenye hizo gatuzi za upinzani.

Kwa kifupi ninashauri utumie muda wako kudadisi taratibu kabla ya kuibuka na kauli zozote.
 
Kuna dada mwingine alijiuzulu August umemsahau. BTW death toll is 67 so far n not 30! According to Kenya's Law society n Amnesty International.
 
Siasa za kenya huzijui kabisa.

Musando aliuawa na mapenzi nje ya ndoa siyo na Uhuru.

Huyu Mama Roseline Akombe na IEBC Chair ni NASA moles sasa ulitegemea nini?

Mauaji hakuna aliyethibitisha hadi leo upande upi wahusika mengine ni wewe wayapika
Wrwe unazijua?acha maneno mingi
 
Siasa za kenya huzijui kabisa.

Musando aliuawa na mapenzi nje ya ndoa siyo na Uhuru.

Huyu Mama Roseline Akombe na IEBC Chair ni NASA moles sasa ulitegemea nini?

Mauaji hakuna aliyethibitisha hadi leo upande upi wahusika mengine ni wewe wayapika

Who are you attempting to fool? Are extrajudicial killings of prominent politicians started yesterday in Kenya? Who killed Dr Robert Ouko? who killed Tom Mboya, Gama Pinto, JM Kariuki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…